Tetesi za soka Ulaya Juni 19, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 19, 2019

19 June 2019 Wednesday 06:28
Tetesi za soka Ulaya Juni 19, 2019


Real Madrid huenda wakamjumuisha kiungo wa kati Mbrazil Casemiro, 27, kwa ofa yoyote ili kumsaini Neymar kutoka PSG. (Marca)

Mlinzi wa England na Manchester United Phil Jones, 27, amepelekwa West Ham kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili Diop. (Sun)

Tottenham wamepewa nafasi ya kumsajili mlinzi wa Sampdoria Joachim Andersen kwa pauni milioni 31.2 baada ya Arsenal kuachana na mpango wa kumsaini kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 23. (Star)

Paris St-German wako tayari kumuuza mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar mwenye umri wa miaka 27 msimu huu. (ESPN)

Everton wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, kutoka Barcelona kwa pauni milioni 22. (Mail)


Manchester United watalazimika kulipa hadi pauni milioni 75 wakitaka kumsajili mlinzi Mfaransa Issa Diop,22 kutoka West Ham, baada ya Red Devils kukataa pendekezo la Hammer la kubadilishana wachezaji katika mkataba utakao mhusisha mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23. (Mirror)

Manchester United wanataka Paul Pogba asiondoka katika klabu hiyo  (Sky Sports)

Hayo yakijiri Real Madrid, wameonywa na rais wao wa zamani, Ramon Calderon kutomsajili Pogba. (Sun)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Leon Goretzka amesema  ''atafurahia sana'' ikiwa klabu hiyo itamsajili winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, msimu huu. (Manchester Evening News)

Ajenti wa Gareth Bale amepuuza madai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid wa miaka 29 huenda akahamia Bayern Munich kwa mkopo. (Mirror)

Manchester City itampati akadarasi rasmi kiungo wa kati wa Valerenga Oscar Bobb atakaporejea Julai 16. (Mail)

Roma wanataka euro milioni 70m sawa na paauni (£62.4m) kumnunua Nicolo Zainiolo, 19, ambaye amehusishwa na uhamisho kwenda Tottenham. (Calciomercato, via Team Talk)

Meneja wa Rangers, Steven Gerrard, 39, amekataa ofa ya  kuwa kocha wa  Derby County kama kinara wao huku mipango ikifanywa kuziba pengolitaloachwa na Frank Lampard anaelekea kujiunga Chelsea. (Times - subscription required)

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumsajili Steve Walsh kama mkurugenzi wa kandanda huku kiungo wa kati wa zamani Darren Fletcher Pia amepewa ofa ya kazi. (Mail)

Southampton wanajiandaa kuipiku Sheffield United na Burnley katika kinyan'ganyiro cha usajili wa mshambuliaji matata raia wa Uingereza Che Adams kwa pauni milioni 14 kutoka Birmingham. (star)

Watford wamewasiliana na PSV Eindhoven katika mpango utakaowezesha kusajiliwa kwa kiungo wa kati wa Uruguay Gaston Pereiro, 24. (Watford Observer)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.