Tetesi za soka Ulaya Juni 20, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 20, 2019

20 June 2019 Thursday 08:23
Tetesi za soka Ulaya Juni 20, 2019

MSHAMBULIAJI wa Paris St-Germain Neymar amekuwa akitafuta nyumba mjini Barcelona, tetesi zinaeleza nyota huyo wa Kimataifa wa Brazil (27) anajiandaa kurejea Nou Camp. (Sport)

Bayern Munich wanajiandaa kujiunga na Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Hispania Rodri, 22, kutoka Atletico Madrid. (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Brazil Jorginho yuko tayari kuondoka Chelsea na kwenda kujiunga na Maurizio Sarri katika klabu ya Juventus ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kusajiliwa kutoka Napoli kwa pauni milioni 50. (Mirror)

Arsenal inapania kumsaini beki wa Celtic raia wa Uskochi Kieran Tierney, 22, msimu ujao. (Mail)

Inter Milan na Atletico Madrid wanataka kumsajili beki wa England anaechezea klabu ya Southampton Ryan Bertrand, 29. (Mail)

Juventus wanaamini wataipiku Real Madrid katika usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mirror)

Sporting Lisbon wanashauriana na Liverpool kuhusu usajili wa winga wa Ureno wa miaka 19, Rafael Camacho. (Standard)

Norwich wanamatumaini ya kumnunua beki wa England Max Aarons, 19, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Manchester United. (Telegraph)

West Ham wameifahamisha Manchester United na Manchester City kuwa hawana mpango wa kumuuza nyota wa Kimataifa wa England anaecheza safu ya kati Declan Rice, 20, msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Chelsea inapania kumuajiri kocha wa Derby Frank Lampard, kama maneja wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu kufikia mwisho wa wiki hii. (Standard)

Manchester United wamekubali kulipa ada ya pauni milioni 55 kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21. (Record)

Hata hivyo madai hayo yamekanushwa huku vilabu hivyo vikiendelea kushauriana kuhusu usajili wa kiungo huyo. (Mail)
Arsenal wanajianda kuweka dau la kumnunua winga wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai, 18. (Football Insider)

Kipa Tom Heaton amekataa ofa ya kandarasi mpya aliyopewa na Burnley. (Guardian)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.