Tetesi za soka Ulaya Juni 24, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 24, 2019

24 June 2019 Monday 06:26
Tetesi za soka Ulaya Juni 24, 2019

Manchester United watatumia kifungo cha sheria cha kumuongezea miezi 12 Marcus Rashford katika kandarasi yake huku kukiwa na hofu kwamba mchezaji huyo (21) huenda akaondoka Man United wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)

Inter Milan haijaafikia kiwango cha £22.3m kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)

Mchezaji wa Leicester City na Uingereza Harry Maguire, 26, anatarajiwa kuwa beki ghali zaidi duniani wiki hii wakati atakapojiunga na Manchester City kwa dau la £80m baada ya kukataa kujiunga na Manchester United. (Mirror)
Manchester United wako katika harakati za kumsaini winga wa Hispania mwenye umri wa miaka 16 Mateo Mejia kwa dau la £600,000 kutoka klabu ya Real Zaragoza. (Sun)

Arsenal inafikiria kumuuza Lucas Torriera, 23, baada ya AC Milan kuwasilisha ombi lao la kwanza kwa kiungo huyo wa Uruguay. (Sport Mediaset, in Italian)

Liverpool na Manchester United watapigania saini ya mchezaji wa Hispania na Real Betis beki wa kushoto Junior Firpo, 22. (Marca)

Newcastle United inatarajiwa kufanya majaribio ya mwisho ili kumzuia mkufunzi wake, Rafael Benitez kuongeza kandarasi yake.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 , ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa mwezi Juni ameripotiwa kupata kazi nchini China. (Evening Chronicle)

Real Betis wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 24. (Estadio Deportivo, in Spanish)

Klabu ya Brighton imekubali kumsajili winga wa Ubelgiji Leandro Trossard, 24, kutoka Genk kwa dau la £18m. (Sky Sports)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool Nicolas Pepe anawaniwa na InterMilan kwa dau la £80m.
Timu hiyo ya Ligi ya Serie A Inter Milan ni miongoni mwa klabu nyingi zilizo na hamu ya kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Lille na Ivory Coast . (L'Equipe, in French)

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amewasilisha ombi la kibinafsi kwa afisa mkuu mtendaji -mwenyekiti Ed Woodward kuharakisha ili kumsajili kiungo wa kati wa Lisbon na Portugal Bruno Fernandes , 24, (Record, in Portuguese, subscription required)

Mkufunzi wa Leicester Brendan Rodgers ameambiwa kwamba anapoteza wakati kujaribu kumsaini kiungo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 26 Callum McGregor kutoka klabu yake ya zamani Celtic. (Scottish Daily Mail)

Klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar imethibitisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Southampton Jordy Clasie, 27. (Daily Echo)

Burnley wamemwambia beki Ben Gibson,26, anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu

Aston Villa ambao wamepanda daraja  ligi ya Premier pamoja na Sheffield United ni miongoni mwa kundi la klabu zilizo na hamu ya kumsaini mchezaji huyo wa Uingereza kwa dau la £15m. (Teamtalk)

Aston Villa wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili beki wa Bournemouth Tyrone Mings,26. Mchezaji huyo wa Uingereza alikuwa kiungo muhimu katika kupandishwa daraja kwa Villa wakati alipoichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.. (Birmingham Mail)

Updated: 25.06.2019 06:36
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.