Tetesi za soka Ulaya Juni 25, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 25, 2019

25 June 2019 Tuesday 06:27
Tetesi za soka Ulaya Juni 25, 2019

Mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, ambaye amecheza misimu miwili kwa mkopo  Bayern Munich, hana uhakika iwapo atarejea katika klabu  ya Bernabeu msimu ujao. (Marca)

Man United itaimarisha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho, (19) iwapo watamuuza Pogba. (Sun)

Kocha wa Juventus Maurizio Sarri anataka kumsajili beki wa kulia wa Tottenham Kieran Trippier, (28) lakini anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Napoli ambao tayari wamewasiliana na mchezaji huyo.. (Mirror)

Paris St-Germain wameipatia ofa Man United ya kubadilishana na mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba. (Independent)

Arsenal itahitaji nusu ya fedha zao ilizotengewa dirisha la uhamisho kumnunua beki wa Celtic raia wa Uskochi Kierna Tierney mwenye umri wa miaka 22 huku mchezaji huyo akiwa na thamani ya £25m kutoka kwa mabingwa hao wa Uskochi.. (Telegraph)

Hatma ya kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 25, katika klabu ya Chelsea haijulikani huku mkopo wake katika klabu ya Real Madrid ukitarajiwa kukamilika mwezi Julai. Klabu hiyo ya Stamford Bridge bado haijamuongezea kandarasi. (Goal)

Neymar hatoruhusiwa kurudi katika klabu yake ya zamani Barcelona kutoka PSG hadi atakapoomba msamaha kwa mabingwa hao wa Hispania na mashabiki wake na kukubali mshahara wake kupunguzwa (El Mundo - in Spanish)

Real Madrid haitakubali maombi ya chini ya paundi milioni 47.7 kumuuza kiungo wa kati wa Hispania Dani Ceballos, ambaye ameivutia  klabu ya Tottenham nchini Uingereza. (AS- in Spanish)
Spurs inamchunguza kinda wa Denmark Andreas Skov Olsen, ambaye anaichezea klabu ya FC Nordsjaelland na ana thamani ya £15m. (Mirror)

Arsenal wanakataa ofa kutoka AC Milan kumuuza kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, 23. (Mirror)

The Gunners wana hamu ya kumsajili winga wa klabu ya Dalian Yifang Yannick Carrasco, lakini bado hawajawasilisha ofa yoyote kwa mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 25 (Football.London)

Aston Villa inataka kumnunua beki wa klabu ya Luton Town na Uingereza James Justin huku klabu ya Leicester pia ikiwa na hamu ya mchezaji huyo. (Birmingham Chronicle)

Beki wa klabu ya Manchester United na Uingereza Axel Tuanzebe, 21, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa anataka hakikisho kuhusu hatma yake katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Sun)

Mchezaji anayewindwa na Arsenal Dominik Szoboszlai, (18) anafikiria kuondoka katika klabu ya Red Bull Salzburg, huku Barcelona na Borussia Dortmund zikimnyatia mchezaji huyo wa Hungary. (Football.London)

Newcastle United haina haja na mshambuliaji wa West Brom na Venezuela Salomon Rondon ambaye alihudumu msimu uliopita akiichezea klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza - licha ya uamuzi wa mkufunzi Rafael Benitez kuondoka katika klabu hiyo. (Star)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.