Tetesi za soka Ulaya Juni 26, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 26, 2019

26 June 2019 Wednesday 08:09
Tetesi za soka Ulaya Juni 26, 2019


Mlinda lango wa zamani wa Itali, Gianluigi Buffon, (41) yuko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kurudi katika klabu ya Juventus kuwa mkurugenzi wa klabu hiyo kutoka PSG ambako alikua katika kandarasi ya mwaka mmoja(Sky Italia via Football Italia)

Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Sevilla na Ufaransa Wissam Ben Yedder (28) uhamisho wake utagharimu  wpaundi  milioni 35.8. (ABC de Sevilla)

Winga wa Itali na Roma Stephan El Shaarawy, 26, amekubali kujiunga na klabu ya China ya Shanghai Shenhua kwa dau la paundi  milioni16.11. (Il Tempo)

Barcelona inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kwa dau la paundi milioni 107 baada ya kifungu cha sheria cha uhamisho wake kuanza kufanya kazi Julai mosi  (Telegraph)
Tottenham Spurs inakaribia kumsajili winga wa klabu ya Leeds United Jack Clarke 18, kwa dau la paundi milioni8.5. Clarke aliichezea klabu hiyo mara 22 msimu wa 2018-19. (Sky Sports)

Napoli huenda ikaanza kuitumia jezi namba 10 ya aliyekuwa nyota wa Argentina Diego Maradona wakijaribu kumvutia mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez kujiunga na timu hiyo. (Daily Mail)

Manchester United inataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa ,15, Mathis Rayan Cherki anayeichezea klabu ya Lyon na ambaye anazivutia klabu kama vile Real Madrid, Juventus, Barcelona na Bayern Munich. (Telegraph)

Tottenham inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Tanguy Ndombele, 22, kwa dau litakalovunja rekodi ya klabu hiyo la paundi milioni 60(Sun)
Mlinda lango wa Liverpool na Ubelgiji Simon Mignolet, 31, anatakiwa na klabu ya Crystal Palace ambao  wameandaa dau la  paundi milioni 8. Mignolet amesalia na kandarasi ya miaka miwili .. (Evening Standard)

Hatahivyo klabu hiyo ya Anfield haiko tayari kumuuza Mignolet kwenda Palace  na itamuachilia kipa huyo iwapo kitita hicho kitakubalika. (ESPN)
Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 31,ana mipango ya kuondoka na kuelekea Uhispania na badala yake wana nyundo hao wameamua kumsajili mshambuliaji wa Uruguay na Celta Vigo Maxi Gomez. (Evening Standard)

Leicester imeshinda harakati za kumsaini beki wa klabu ya Luton na Uingereza James Justin kwa dau la paundi milioni 8 ikiwashinda Aston Villa na mabingwa wa ligi ya Uskochi kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mirror)

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, ambaye alifunga katika ushindi wa Liverpool dhidi ya Tottenham katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya anasakwa na klabu ya Real Betis, huku klabu hiyo ya Hispania ikiandaa dau la paundi milioni 10 kumnunua mchezaji huyo wa Ubelgiji . (BeIn Sports - in French)

Updated: 27.06.2019 07:03
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.