Tetesi za soka Ulaya Juni 28, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 28, 2019

28 June 2019 Friday 06:22
Tetesi za soka Ulaya Juni 28, 2019

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, anahitajika na Manchester United, anaonekana kukaribia kuondoka katika klabu ya PSG baada mamake kufichua kwamba hakuna klabu iliowasilisha ofa yoyote kwa mwanawe(Daily Mail)

Arsenal inataka kumsajili mshambuliaji wa Monaco Keita Balde, 24, baada ya inter Milan kujiondoa katika harakati za kumsajili mchezaji huyo wa Senegal . (Le 10 Sport, via Metro)

Manchester United inataka kumnunua beki wa Ufaransa na Barcelona Samuel Umtiti, (25). (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, (23) anasalia kuwa mchezaji anayehitajika sana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich msimu huu licha ya mpango huo kusita hapo awali. (Sky Sports)

Mkufunzi wa klabu ya Sporting Marcel Keizer anaamini kwamba nafasi ya kumzuia kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandez katika klabu hiyo ni ndogo, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zimevutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 (Record, via Manchester Evening News)

Mkufunzi wa Celtic Neil Lennon ameambia Arsenal watahitajika kulipa zaidi iwapo wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Uskochi Kieran Tierney, 22. (Telegraph)

Beki wa Borussia Dortmund na Ufaransa,20 Dan-Axel Zagadou, anataka kuondoka katika klabu hiyo na ananyatiwa na Arsenal. (Bild, via Mirror)

Babake mshambuliaji wa Juventus Moise Kean, 19, ametangaza kwamba raia huyo wa Itali anataka kuhamia Inter Milan". (Mirror)

Atletico Madrid inafikiria kumsajili mchezaji wa Real Madrid na Colombian James Rodriguez, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa ahitajiki tena Real Madrid. (Cadena SER, via AS)

Tottenham iko tayari kumnunua mchezaji anayelengwa na Arsenal William Saliba, huku klabu ya St-Etienne ikisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ana thamani ya  paundi  milioni 20. (RMC, via Star)

Bayern Munich ilijaribu kuteka uhamisho wa beki wa klabu ya PEC Zwolle Sepp van den Berg kuelekea Liverpool wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 kutoka Uholanzi alikuwa akifanyiwa uchunguzi wa afya. (Times)

Naibu mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola ataondoka Chelsea wikendi hii wakati ambapo kandarasi yake itakuwa inakamilika baada ya kukataa ofa ya kuwa balozi wa klabu hiyo. (Guardian)
Mchezaji wa Real Madrid na Norway Martin Odegaard, 20, anatarajiwa kuondoka kwa mkopo kwa kipindi cha misimu mingine miwili (AS)

Kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, 21, anatarajiwa kuripoti kwa mazoezi ya kujiandaa kwa msimu kama kawaida wiki ijayo licha ya kulengwa na Man United. (Chronicle)

Beki wa Arsenal na Poland Krystian Bielik anataka kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu . (Sun)

Mshambuliaji wa Ujerumani Bassala Sambou, 21, amekataa kandarasi mpya na klabu ya Everton na anatarajiwa kuhamia Ujerumani ama Eredivisie. (Liverpool Echo)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Expeditho Msamba 2019-06-28 21:58:55

Thanks for the updates, but why Man uyd they are too slow to sign the players.. As a member ,and saporter and fan of uyd,im not filing happy for that. Edwood please hive the cash to Ole...please do something for utd...