Tetesi za soka Ulaya Juni 7, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 7, 2019

07 June 2019 Friday 09:06
Tetesi za soka Ulaya Juni 7, 2019

MSHAMBULIAJI wa Brazil, Neymar amekataa kuelekea Real Madrid na kuiambia Paris Saint-Germain kuwa anataka kuelekea Barcelona tu . (Express)


Everton wameiambia Tottenham wanamtaka beki wa kushoto Danny Rose, 28, ili kumuachia Lucas Digne, 25,aondoke Goodison Park. (Star)


Tottenham imepewa ofa ya mchezaji wa kijerumani na mshambuliaji wa Paris St-Germain,Julian Draxler,25, kama mbadala wa Christian Eriksen ikiwa mchezaji huyo, 27, ataondoka. (Star)
Beki wa kulia wa Juventus na Ureno, Joao Cancelo, 25, anaweza kuwa njiani kuelekea Manchester City kwa gharama ya pauni milioni 44- ikiwa the blues wanamuuza beki wa pembeni Danilo, 27.(Goal)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Matthijs de Ligt, 19 huenda akachagua kuichezea Paris St-Germain au Barcelona. (Marca)

Mashetani wekundu wanalenga sahihi mbili kubwa mwezi huu.(Sun)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Leicester City na Uingereza, Harry Maguire, 26,anajiandaa kuikacha Manchester United, na kuwa na mpango wa kwenda Manchester City. (Mail)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans,22, ambaye alitumia msimu uliopita akiichezea Leicester City kwa mkopo akitokea Monaco, anahitajika Old Trafford ikiwa Paul Pogba, ataamua kuondoka United.(Independent)
Kiungo wa kati wa Leicester City, James Maddison anataka kuendelea kubaki King Power, ingawa Manchester United na Tottenham zina nia ya kumchukua. (Mail)

Paris Saint-Germain huenda wakatoa ofa kumnasa kiungo wa kati wa Everton, Idrissa Gueye. (Le 10 Sport)
Winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, karibu atahamia Arsenal kutoka timu ya Dalian Yifang ya uchina.(Mirror)

Mchezaji wa nafasi ya Joachim Andersen,23, huenda akachagua kwenda AC Milan badala ya Arsenal kama meneja wake wa timu anayoichezea sasa Sampdoria, Marco Giampaolo ataamua kuelekea Rossoneri. (Metro)

Schalke wako kwenye kinyang'anyiro cha kupata saini ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Everton Jonjoe Kenny,22, kwa mkopo.(Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 29, anajiandaa kuzungumza na Fenerbahce baada ya mipango ya Newcastle kumpata kwa mkopo kutoka West Brom kugonga mwamba. (Sun)

Updated: 07.06.2019 09:15
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.