Tetesi za soka Ulaya Juni 8, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 8, 2019

08 June 2019 Saturday 11:49
Tetesi za soka Ulaya Juni 8, 2019

Barcelona itamwania mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, (21) iwapo itashindwa kumsajili Antoine Griezmann au Neymar. (Mail)

Atletico Madrid inataka kumsajili beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, ili kumrudisha nyumbani  (Goal)

Real Madrid itafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, badala ya kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba. (Independent)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri ataweka saini kandarasi ya miaka mitatu ili kuchukua wadhfa wa kuifunza Juventus wiki ijayo (Guardian)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25, anahitajiwa na Manchester United. (Times - subscription required)

Barcelona imekataa ripoti kwamba itamnunua kipa Gianluigi Buffon baada ya mchezaji huyo(41) kutangaza  ataondoka Paris Saint Germain mwisho wa msimu huu (Mundo Deportivo - in Spanish)

Buffon anataka kustaafu katika soka baada ya kushinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki akiichezea Itali katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini Japan(Gazzetta dello Sport, via Mail)

Mchezaji wa Fulham na Uingereza Ryan Sessegnon, 19, ameiambia klabu hiyo hatosaini kandarasi mpya na kwamba anaelekea Tottenham (Guardian)

Liverpool itashindana na Tottenham na Manchester United katika kumsaini kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 24 na raia wa Ureno Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon. (Record, via Mirror)

Winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe atakataa ombi la kucheza katika ligi ya Uingereza na badala yake kuelekea Bayern Munich. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ananyatiwa na Liverpool na Manchester United. (Sun)
Arsenal wameambiwa watalazimika kuilipa Sampdoria £44m ili kumnunua beki wa Italia, Joachim Andersen na winga wa Ubelgiji Dennis Praet, 25. (Star)

West Ham wanamnyatia mchezaji wa  Newcastle na nyota wa Uingereza 21 Isaac Hayden, 24. (Star)

Everton imejiunga na Arsenal katika harakati za kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 27 beki wa Togo, Djene Dakonam kutoka Getafe. (Marca - in Spanish)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.