Tetesi za soka Ulaya Juni 9, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 9, 2019

09 June 2019 Sunday 14:12
Tetesi za soka Ulaya Juni 9, 2019

Manchester United inataka kumsajili kwa mkopo winga wa Real Madrid raia wa Wales Gareth Bale, 29. (Sunday Mirror)


Man United bado wana mpango wa kumsajili beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26, pia beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Sunday Express)


Arsenal wapo karibu kuwasajili wachezaji wawili kutoka klabu ya Sampdoria ya Italia kiungo Mbelgiji Dennis Praet, 25, na beki wa kati raia wa Denmark Joachim Andersen, 23. (Gazzetta dello Sport, via Talksport)

Kocha Jose Mourinho amewaambia rafiki zake kuwa anaweza kwenda kuifunza klabu ya Newcastle na yupo tayari kufanya mazungumzo na anayetarajiwa kuinunua klabu hiyo Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan. (Sunday Mirror)

Kiungo wa England Jesse Lingard, 26, anakaribia kuongeza mkataba na kupata mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester United. (Sun on Sunday)

Manchester United wamepeleka dau la pauni milioni 84 kwa klabu ya Napoli wakitaka kumsajili beki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (Corriere dello Sport, via Mail)

Tottenham wanatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 40 ili kumsajili mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Sun on Sunday)

Liverpool wapo tayari kumuuza winga wao raia wa Wales Harry Wilson, 22, kwa dau la pauni milioni 21. Winga huyo aliitumikia kwa mkopo klabu ya Derby msimu uliopita. Klabu mbili za Ujerumani Hoffenheim na RB Leipzig zinaripotiwa kumnyemelea winga huyo. (Sunday Mirror)

Golikipa mkongwe wa Italia Gianluigi Buffon, 41, anaweza kurejea kwenye klabu yake ya kwanza Parma baada ya kutangaza kuwa ataachana na klabu ya Paris St-Germain. (La Gazzetta dello Sport, via Goal - in Italian)

David Beckham anataka beki wa kulia raia wa Ecuador Antonio Valencia, 33, tajiunge na klabu yake ya Inter Miami ya nchini Marekani. Valencia ameondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wake na Mashetani hao Wekundu. (Sun on Sunday)

Rais wa klabu ya Benfica Luis Filipe Vieira amesema namna pekee ya klabu hiyo kumbakiza mshambuliaji wao kinda na nyota Joao Felix, 19, ni kwa kumuuza kisha kumuomba kwa mkopo msimu ujao. Klabu za Manchester United na Manchester City tayari zinamuwinda mchezaji huyo raia wa Ureno. (Sunday Mirror)

Kiungo wa Manchester United na Brazil Andreas Pereira, 23, anakaribia kusaini nyongeza ya mkataba kwa miaka minne na klabu hiyo yenye maskani yake katika uga wa Old Trafford. (Sun on Sunday)
Kiungo wa klabu ya Chelsea na Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, anataka kubaki Chelsea msimu ujao baada ya kutolewa kwa mkopo msimu uliopita katika klabu ya AC Milan. (L'Equipe - in French)

Updated: 09.06.2019 14:17
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.