Tetesi za soka Ulaya Mei 17, 2019

"Mchezaji wa Manchester United Marcus Rashford( 21) na wachezaji wawili wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, wanyemelewa na Barcelona"

Tetesi za soka Ulaya Mei 17, 2019

"Mchezaji wa Manchester United Marcus Rashford( 21) na wachezaji wawili wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, wanyemelewa na Barcelona"

17 May 2019 Friday 09:31
Tetesi za soka Ulaya Mei 17, 2019

Manchester United itafaidi £15m iwapo Crystal Palace itamuuza Zaha msimu huu wa joto kutokana na kifungu katika mkataba kuhusu kumuuza winga huyo wake wa zamani. (mail)


Real Madrid inatarajiwa kujaribu tena kuwasilisha ombi kwa Liverpool msimu huu wa joto kumsajili mshambuliaji raia wa Misri Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 26. (Canal+, kupitia Mail)

Mlinzi raia wa Uhispania wa Chelsea Marcos Alonso, mwenye umri wa miaka 28, anapigwa jicho na Atletico Madrid. (AS, kupitia Sun)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic, aliye na umri wa miaka 21, anakaribia kukamilisha uhamisho wa thamani ya £52.4m kwenda Real Madrid. (Sky Sports)


Barcelona inapanga kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, aliyetangaza mipango ya kutaka kuondoka Atletico Madrid. (Goal.com)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, na wachezaji wawili wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, aliye na miaka 29, na Alexandre Lacazette, wa miaka 27, ni wachezaji ambao wanaweza kulengwa na Barcelona. (Mundo Deportivo)

Mchezaji wa kiungo cha mbele raia wa Ujerumani anayeichezea Bayer Leverkusen Julian Brandt, mwenye umri wa miaka 23, huenda akazisusia timu mbili zilizo katika fainali za ubingwa wa Ulaya Tottenham na Liverpool ili kusalia Ujerumani. (Sky Germany, kupitia Mirror)

Matumaini ya mshambuliaji wa West Brom mwenye umri wa miaka 29 Salomon Rondon kupata uhamisho wa kudumu kwenda Newcastle kunategemea Rafa Benitez kusalia kuwa msimamizi huko St James' Park. (Newcastle Chronicle)

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo anasema mchezaji anayelengwa na Manchester City Rodrigo, mchezaji wa kiungo cha mbele wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto iwapo tu atataka mwenyewe kuondoka. (Manchester Evening News)

Kaimu mwenyekiti mtendaji wa Manchester United Ed Woodward amekiri kutumia uzito wa fedha wa klabu hiyo kumsaidia Ole Gunnar Solskjaer kuijenga upya klabu hiyo baada ya msimu uliokuwa na 'mtikisiko'.(Sky Sports)

Ajenti wa mchezaji wa Atletico Madrid raia wa Ghana Thomas Partey, mwenye umri wa miaka 25, amebainisha dau la mchezaji huyo huku kukiwepo taarifa za Manchester United kutaka kumsajili. (Manchester Evening News)

Wolves inapanga uhamisho wa msimu wa joto wa mchezaji wa Reading mwenye umri wa miaka 18 Danny Loader. (Football Insider, kupitia Birmingham Mail)
Aliyekuwa mwenyekiti wa Crystal Palace Simon Jordan anaamini Eagles wanapswa kumuuza Wilfried Zaha msimu huu wa joto na anasema £60m ni thamani ya wastani kwa mchezaji huyo wa miaka 26 raia wa Ivory Coast. (Talksport)
Updated: 17.05.2019 10:02
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.