Tetesi za soka Ulaya Mei 18, 2019

Tetesi za soka Ulaya Mei 18, 2019

18 May 2019 Saturday 08:08
Tetesi za soka Ulaya Mei 18, 2019

Juventus wanamtaka meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino. (Express)  

Pia Juventus wamewasiliana na meneja wa Chelsea Maurizio Sarri baada ya kutangazwa kwa taarifa ya kuondoka kwa Massimiliano Allegri hivi karibuni. (SNAI, via Express)

Sarri atasubiria  uamuzi kutoka kwa Chelsea kuhusu msimamo wao baada ya fainali ya Ligi ya Ulaya kwani mikataba ya wakufunzi wake wote inamalizika na iwanahitaji kujua wazi hatma zao. (Times)

Mshambuliaji wa England Marcus Rashford (21), anataka hakikisho kutoka kwa Manchester United kabla ya kukubali mkataba mpya.(Sun)

Manchester United wamewasiliana na Fulham juu ya uwezekano wa kusaini mkataba na mlinzi Ryan Sessegnon(19) siku ya Jumapili, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akilengwa na Tottenham. (Sky Sports)
Mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool Muingereza Adam Lallana, mwenye umri wa miaka 31, anafikiria kwa makini kurejea Southampton. (Express)

Everton wanapanga dau la £35m kwa ajili ya mshambuliaji wa Bournemouth Muimngereza Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 27, lakini hawakutaka kulazimishwa kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 29, kwa mkataba wa pesa. (Sun)

Manchester United bado wanataka kusaini mkataba na nahodha wa Ajax Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19. (Telegraph)

Newcastle na Rafa Benitez wako tayari kuendelea na mazungumzo juu ya hali ya baadae ya meneja wikendi hii, huku, wakiwa pande hizo mbili zikiwa bado hazijafikia makubaliano. (Newcastle Chronicle)

Wakili wa mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, anatarajia kukutana na maafisa wa klabu ya Barcelona ili kukamilisha mpango wake wa kuhamia timu hiyo . (Marca)

Griezmann ataondoka Atletico Madrid msimu huu lakini Manchester City na Paris St-Germain wameachana na mpango wa kumchukua mshambuliaji huyo (independent)

Manchester City wamewasilisha ombi rasmi kwa kiungo wa kati wa Atletico Madrid Rodri, mwenye umri wa miaka 22 wakimtaka ajiunge na klabu hiyo. (AS)

Duru kutoka Newcastle zimesisitiza kuwa mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Uingereza Sean Longstaff, anahamia Manchester United, hayuko katika mpango wao wa mauzo msimu huu. (Newcastle Chronicle)

Chelsea wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Ajax Mbrazil David Neres, mwenye umri wa miaka 22, kwasababu wanamatumaini kuwa marufuku ya vipindi vyao viwili vya uhamisho itakuwa imetatuliwa na mahakama ya utatuzi wa mizozo ya michezo. (Star)

Everton wamefanya mazungumzo juu ya rasimu ya mkataba kwa ajli ya mlindalango wa Denmark goalkeeper Jonas Lossl, mwenye umri wa miaka 30, ambaye yuko huru baada ya kuachiliwa na Huddersfield. (Mail)

Wayne Rooney amewashutumu wachezaji wa Manchester United kwa "kutafuta mtu wa kumlaumu" kila mara wanapokuwa juu ama chini kimchezo na anasema kikosi kinahitaji kuanza kumuogopa Ole Gunnar Solskjaer. (Mirror)

Everton wametoa orodha ya wachezaji wanaowalenga ikiwa watashindwa kusaini mikataba ya jumla kwa wachezaji Andre Gomes,mwenye umri wa miaka 25 na Kurt Zouma,mwenye umri wa miaka 24, ambao kwa sasa wanachezea timu hiyo kwa mikataba ya mikopo. (Liverpool Echo)

Norwich wanamfuatilia kwa karibu nahodha wa Hannover Mjerumani Marvin Bakalorz, mwenye umri wa miaka 29 anayecheza safu ya kati . (Eastern Daily Press)

Aston Villa wamemteua meneja wa zamani wa Notts County boss -Ian McParland kama meneja mpya wa kikosi. (Birmingham Mail)

Meneja msaidizi wa Rangers Gary McAllister amemuonya mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, mwenye umri wa miaka 22, kwamba anahitaji kujifunza kutokana na matendo yake ili kuboresha rekodi yake ya nidhamu iliyoiweka hatima yake mashakani ha . (Express)

Liverpool wamemuonya kuwa shabiki wao yeyote atakayepatikana akiuza tiketi za fainali za Championi Ligi kupitia njia zisizo rasmi atakabiliwa na marufuku ya kutoshuhudia mechi katika Anfield. (Liverpool Echo)

Arsenal wanawataka wachezaji Tyreece John-Jules na Xavier Amaechi wote wenye umri wa miaka 18 wasaini mikataba, huku Waingereza hao wakilengwa na klabu ya Bayern Munich na klabu nyingine za Ujerumani. (Goal.com)
Updated: 19.05.2019 07:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.