Tetesi za soka Ulaya Mei 19, 2019

"Paris St-Germain wamejidhatiti kumsajili kiungo mkabaji wa Ufaransa na Chelsea N'Golo Kante, 28 katika kipindi hiki cha usajili"

Tetesi za soka Ulaya Mei 19, 2019

"Paris St-Germain wamejidhatiti kumsajili kiungo mkabaji wa Ufaransa na Chelsea N'Golo Kante, 28 katika kipindi hiki cha usajili"

19 May 2019 Sunday 13:54
Tetesi za soka Ulaya Mei 19, 2019
KLABU ya Paris St-Germain wapo tayari kumsubiria kipa wa Manchester United David de Gea, 28, amalizie mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake kisha wamsajili bure kama mchezaji huru. (Sunday Express)

Klabu ya Manchester City wanapigiwa chapuo la kumsajili kiungo mkabaji wa Atletico Madrid Rodrigo, 22, lakini ilikukamilisha usajili huo, kocha wa City Pep Guardiola yawezekana akamuuza streka wake raia wa Gabriel Jesus, 22. (Sun on Sunday)

Crystal Palace wanataka walipwe dau la uhamisho la pauni milioni 60 kwa beki wao wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 21. Dau hilo linaonekana kuwekwa ili kuwazuia Manchester United ambao wanamtaka mchezaji huyo. (Mail on Sunday)


Manchester United wanahakika kuwa mshambualiaji wao Marcus Rashford, 21, atasaini mkataba mpya utakaomuwezesha kulipwa kitita cha pauni 300,000 kwa wiki, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara tatu ya kile anacholipwa kwa sasa. (Star on Sunday)

Arsenal wapo tayari kumsajili mshambuliaji Alexis Claude-Maurice, 20, kutoka klabu ya Lorient ambaye pia amekuwa akinyemelewa klabu ya Norwich ambayo imepanda daraja. (Sunday Express)
Kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26, yupo tayari kukatwa mshahara ili ajiunge na klabu ya Real Madrid. (Manchester Evening News)


Klabu ya Leicester imewatuma waangalizi wake kumchunguza mshambuliaji wa klabu ya AC Milan raia wa Uturuki Hakan Calhanoglu, 25. (Gazzetto dello Sport, via Leicester Mercury)

Chelsea watampatia jezi namba 10 winga wake raia wa England Callum Hudson-Odoi, 18, ambayo imeachwa na Eden Hazard, ikiwa ni moja ya njia ya kumshawishi mchezaji huyo kinda kusaini mkataba mpya utakaomfanya asalie klabuni hapo. (Mail on Sunday)

Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha 26, lakini wapo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 40 tu, ambacho ni nusu ya kiwango ambacho Palace wanadhamiria kumuuza mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Ivory Coast. (Sun on Sunday)

Matakwa ya ajenti Mino Raiola yanatatiza harakati za uhamisho wa beki kisiski na kinda wa Ajax Matthijs de Ligt, 19. (Mundo Deportivo, via Sunday Mirror)

Paris St-Germain wamejidhatiti kumsajili kiungo mkabaji wa Ufaransa na Chelsea N'Golo Kante, 28 katika kipindi hiki cha usajili. (Sunday Mirror)

Tottenham wanaweza kumsajili kocha wa Juventus Massimiliano Allegri endapo kocha wao Mauricio Pochettino ataihama klabu hiyo. (Sunday Express)

Pochettino anatakiwa na miamba ya Italia Juventus na miamba ya Ujerumani Bayern Munich. (Star on Sunday)

Winga Gareth Bale, 29, kiungo Dani Ceballos, 22, kipa Keylor Navas, 32, na kiungo Marcos Llorente, 24, wote wanatarajiwa kuihama klabu ya Real Madrid katika kipindi hiki cha dirisha la usajili. (Marca)
Updated: 20.05.2019 06:23
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.