Tetesi za soka Ulaya Mei 21, 2019

"Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazilia Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29"

Tetesi za soka Ulaya Mei 21, 2019

"Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazilia Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29"

21 May 2019 Tuesday 09:18
Tetesi za soka Ulaya Mei 21, 2019
Manchester United wanatarajiwa kutangaza dau la  euro milioni 160 (£138m) kumuuza kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba (26). (Star)

Juventus wameachana na Conte na sasa wanamlenga meneja wa sasa wa Chelsea, Maurizio Sarri. (Sun)

Mlinzi wa Leicester na nyota wa kimataifa wa England Harry Maguire  (26) ni mmoja wa walinzi wa kati wanaolengwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Vincent Kompany. (Sky Sports)


Bayern Munich wanaamini watamsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ujarumani Leroy Sane  (23) kutoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mirror)

Meneja mpya wa Anderlecht, Kompany anamfuatilia kwa karibu kocha wa chuo mpira cha Manchester City, Simon Davies na mkuu wa sayansi ya michezo Sam Erith, kuungana nae mjini Brussels. (Telegraph)

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameafiki masharti ya kujiunga na Inter Milan kama kocha wao mpya msimu ujao. (Guardian)

Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazilia Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29. (Star)


Nyota wa zamani wa kimataifa wa Argentina Gabriel Batistuta, 50, bado hajafikia kiwango cha ukufunzi wa timu kubwa lakini sasa inaaminiwa kuwa ameonesha nia ya kuchukua nafasi ya usimamizi iliyoachwa wazi katika klabu ya Middlesbrough. (Hartlepool )

Chelsea wanatarajiwa kuthibitisha kuwa mshambuliaji wa kimataifa Ufaransa Olivier Giroud, 32, amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mmoja mwingine. (London Evening Standard)

Meneja wa Ireland Kaskazini Michael O'Neill amaeibuka moja wa watu wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya umeneja iliyoachwa wazi West Brom. (Express and Star)

Meneja mkuu wa Hertha Berlin Michael Preetz amefanya mazungumzo na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp katika juhudi za kutafuta huduma za kiungo wa kati wa kimataifa wa Serbia Marko Grujic, 23, kwa mkopo wa mwaka mwingine tena. (Liverpool Echo)

Mlinzi mahiri wa zamani wa Brighton Bruno, 38, anasomea kozi ya ukufunzi wa Uefa mjini Belfast. (Argus)

Updated: 22.05.2019 04:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.