Tetesi za soka Ulaya Mei 22, 2019

"Kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, atapewa jukumu la unahodha wa klabu hiyo katika juhudi za kumshawishi Mfaransa huyo asiondoke Old Trafford"

Tetesi za soka Ulaya Mei 22, 2019

"Kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, atapewa jukumu la unahodha wa klabu hiyo katika juhudi za kumshawishi Mfaransa huyo asiondoke Old Trafford"

22 May 2019 Wednesday 08:51
Tetesi za soka Ulaya Mei 22, 2019
Tottenham wamesimamisha mpango wao wa kumsajili winga wa Crystal Palace Wilfred Zaha (26) baada ya kushindwa kufika bei ya pauni milioni mia moja (£100m) kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast . (Evening Standard)

Kipa wa Hispania na Manchester United David de Gea (28) amekataa kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo wakati mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)


Antonio Conte ameshinda makabiliano ya kisheria dhidi ya Chelsea na the Blues sasa ni lazima wamlipe meneja wao wa zamani £9m kama fidia ya kumfuta kazi msimu uliyopita. (Times - subscription required)

Meneja wa Derby County, Frank Lampard atajaribu kumsajili mchezji mwenzake wa zamani katika klabu Chelsea, Gary Cahill ikiwa watainyuka Aston Villa katika mechi ya champions Jumatatu ijayo itakayowapandisha  daraja hadi ligi kuu ya England msimu wa mwaka 2018-19. (Mirror)

Kipa wa Arsenal Petr Cech (37) atarejea Chelsea msimu huu wa joto kuchukua wadhifa wa mkurugenzi wa michezo. (Sky Sports)

Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsaini winga wa Swansea na Wales, Daniel James, 21 kwa pauni milioni kumi na tano.(Mail)

Gunners wanatafakari uwezekano wa kumsajili kwa uhamisho wa bila malipo kipa wa Dynamo Dresden na Ujerumani wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Markus Schubert, 20, msimu ujao kuchukua nafasi ya Cech. (Bild - in German)

United watalazimika kulipa pauni milioni hamsini (£50m) kumpata beki wa Crystal Palace Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 21, ambaye   Ole Gunnar Solskjaer amemteua kama mchezaji bora atakaye boresha safu ya nyuma ya timu yake msimu ujao. (Mirror)

Newcastle na West Ham wanapani akumsajili mshambuliaji wa klabu ya Brugge Mbrazil Wesley Moraes, 22. (Mirror)

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri, ananyatiwa  na klabu ya Roma. (Sky Sports)


The Blues hawatazuia Sarri kuondoka ikiwa Juventus itakuwa tayari kulipa hadi pauni milioni tano (£5m) kama fidia ya kumrudisha Italia. (Telegraph)

Spurs wamefanya mazungumzo ya kumsaini mshambuliaji wa Celta Vigo raia wa Uruguay Maxi Gomez, 22, ambaye mkataba wake unamruhusu kuondoka kwa euro milioni arubaini na tatu(£43m). (Star)


Kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, atapewa jukumu la unahodha wa klabu hiyo katika juhudi za kumshawishi Mfaransa huyo asiondoke Old Trafford. (ESPN)
Updated: 23.05.2019 08:51
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Swagger Boy 2019-05-31 16:59:05

Sgio Mane Tetes Ana Talajiwa Kwenda Clab Gan

Avatar
KENEDY SADOCK SEIPH 2019-06-03 12:22:11

is better for man u to release paul pogba to juventus for exhange with dybala