Tetesi za soka Ulaya Mei 27, 2019

"Kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amesema hana hakika kama washambuliaji wake raia wa Brazil Neymar na Mfaransa Kylian Mbappe kama watabakia"

Tetesi za soka Ulaya Mei 27, 2019

"Kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amesema hana hakika kama washambuliaji wake raia wa Brazil Neymar na Mfaransa Kylian Mbappe kama watabakia"

27 May 2019 Monday 08:58
Tetesi za soka Ulaya Mei 27, 2019


MSHAMBULIAJI wa Spurs Harry Kane anatarajiwa kusafiri na wachezaji wenzake kulekea jijini Madrid pamoja na kikosi kizima cha klabu yake. Kane anajaribu kuthibitisha kuwa yupo 'fiti' kuchuana na Livepool kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool. (Mail)

Kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amesema hana hakika kama washambuliaji wake raia wa Brazil Neymar, 27, na Mfaransa Kylian Mbappe, 20, kama watabakia na klabu yake msimu ujao ingawa bado anawahitaji. (Sky Sports)


Kocha wa zamani wa Manchester United, Jose Mourinho bado hajafanya uamuzi wa klabu gani ya kwenda kuifundisha toka alipofukuzwa na United mwezi Disemba, 2018. (Sky Sports)

Kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante, 28, anaweza kuukosa mchezo wa fanali wa Europa dhidi ya Arsenal baada ya kupata majeraha ya goti akiwa mazoezini. (Guardian)

Mchezaji anayewaniwa na Barcelona Matthijs de Ligt, 19, ataamua mustakabali wake baada ya kushiriki ligi ya kimataifa ya Ulaya na timu yake ya taifa ya Uholanzi - tayari beki huyo kisiki na nahodha wa Ajax amesema anaipenda ligi ya Primia. (ESPN)


Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley amekubali kuiuza klabu yake kwa binamu wa wa mmiliki wa Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 305. (Sun)

Klabu ya Manchester City wameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Monaco mwenye thamani ya pauni milioni 40, Youri Tielemans. Klabu ya Leicester pia wanataka kumsajili kiungo huyo raia wa Ubelgiji mwenye miaka 22 baada kuichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita. (Sun)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kumbakiza beki Sergio Ramos (33) klabuni hapo msimu ujao. Klabu kadhaa zinamuwinda beki huyo mkongwe zikiwemo Liverpool, Manchester United na timu kadhaa za ligi ya Uchina. (Marca - in Spanish)

Timu ya Stoke City imemtaarifu mshambuliaji wao raia wa Burundi Saido Berahino mwenye thamani ya pauni milioni 12 kuwa wamesitisha mkataba wake baada ya kukutwa na kosa la kuendesha gari huku akiwa amekunywa pombe. (Mail)

Klabu ya Tottenham wamearifiwa kuwa itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 20 ili kumsajili kiungo kinda wa England anayechezea Leeds United Jack Clarke, 18. (Mirror)

Beki raia wa Argentina Marcos Rojo, 29, amesema kuwa amehakikishiwa mustakabali wake na uongozi wa klabu ya Manchester United. (Express)
Rais wa klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness amemwambia beki mkongwe wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani Jerome Boateng, 30, kuwa anaweza kuihama klabu hiyo ya Bundesliga. (Bild - in German)

Raia wa Algeria na mchezaji wa zamani wa Newcastle Mehdi Abeid  (26) anataka kurejea kwenye ligi ya Primia badala ya kusaini mkataba mpya na klabu ya Dijon kwenye Ligi ya Ufaransa. (L'Equipe - in French)

Updated: 27.05.2019 16:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.