Tetesi za soka Ulaya Oktoba 11, 2019

Tetesi za soka Ulaya Oktoba 11, 2019

11 October 2019 Friday 06:57
Tetesi za soka Ulaya Oktoba 11, 2019

KOCHA wa Everton Marco Silva amepewa michezo mitatu ya kubadili hali ya mambo ama atimuliwe kazi. (Star)

Beki wa Barcelona Gerard Pique, 32, alikaribia kuinunua klabu ya Notts County mwishoni mwa msimu uliopita. (ESPN)

Kocha wa Juventus Maurizio Sarri anataka kumsajili beki wa kushoto Mtaliano Emerson, 25, kutoka Chelsea. (Express)

Jose Mourinho amekataa ofa ya kuifundisha klabu ya Lyon kwa kuwa ameshapata klabu nyingine, hayo ni kwa mujibu wa rais wa ligi ya Ufaransa, Jean-Michel Aulas. (Goal)

Manchester United inajipanga kulipa kitita cha paundi milioni 130 kuwanyakua wachezaji wawili wa Leicester na England; mlinzi Ben Chilwell na kiungo James Maddison, wote wana miaka 22. (Sun)

Hata hivyo kuna ripoti zinadai kuwa klabu ya Chelsea kwa sasa ndio wanapigiwa upatu zaidi kumnasa beki wa kushoto Chilwell baada ya marufuku dhidi yao ya usajili itakapokwisha. (Mail)

Manchester United wanataka kusajili wachezaji wapya nane katika kipindi cha misimu miwili ijayo na tayari wameshaandaa orodha ya wachezaji hao. (Telegraph)

Real Madrid hawataki kupoteza bahati kwa kutomsajili kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, mpaka mwisho wa msimu ambapo kuna uwezekano akaongeza mkataba na klabu yake ya Tottenham. (Marca)

Tottenham pia wana matumaini kuwa watamuuza Eriksen mwezi Januari ili kuzuia wasimpoteze bure mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utakuwa unaisha. (Mirror)

Japo rais wa Real Madrid Florentino Perez anataka kumsajili Eriksen, kipaumbele cha kocha Zinedine Zidane bado ni kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26. (ESPN)

Manchester City wanatafakari juu ya kufanya usajili wa mwezi Januari kwa kumnunua beki wa timu ya Benfica Ruben Dias, 22, ambaye pia anahusishwa na uhamisho kuelekea Manchester United. (Mirror)

Arsenal wanamfuatilia kwa karibu kiungo kinda wa klabu ya Feyenoord ya Uholanzi Orkun Kokcu,18, mwenye thamani ya pauni milioni 20. (Mail)

Sampdoria wanakaribia kumteua kocha wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri, 67, kama kocha wao mpya. (Tuttosport - in Italian)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa klabu ya Rostov na raia wa Norway Mathias Normann, 23, mwezi Januari. (Goal)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.