Tetesi za soka Ulaya Oktoba 22, 2019

Tetesi za soka Ulaya Oktoba 22, 2019

22 October 2019 Tuesday 06:56
Tetesi za soka Ulaya Oktoba 22, 2019

MENEJA wa Italia Roberto Mancini huenda akamjumuisha kipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon, 41, na kiungo wa kati wa Boca Juniors wa miaka 36 Daniele de Rossi katika kikosi cha Yuro 2020. (Rai Sport via Mail)

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema anataka kubakia klabuni hapo maisha. (Marca)

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anasema kuwa anahofia kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo (Mirror)

Barcelona imemaliza mzozo wake na Atletico Madrid kuhusu usajili wa Antoine Griezmann, 28, kwa kulipa Yuro milioni 15 zaidi kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (El Mundo - in Spanish)

Klabu ya Derby Country itampatia nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, mafunzo maalum kuhakikisha yuko tayari kwa mashindano atakapojiunga na klabu hiyo kutoka DC United. (Mail)

Kiungo wa kati wa Brazil na Manchester United Fred, 26 - ambaye alinunuliwa kwa paundi milioni 47 kutoka Shakhtar Donetsk mwezi Juni 2018 - anaamini kuwa ameanza kupata uzoefu wa soka la Uingereza. (Telegraph)

Juventus na Atletico Madrid zinamfuatilia beki wa West Brom wa miaka 19, Nathan Ferguson.(Sun)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, anatakiwa na Crystal Palace na huenda akajiunga na klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Daily Star)

Beki wa zamani wa Arsenal na England Sol Campbell, 45, anafanya mazungumzo ya kuwa mkufunzi wa Southend, inayoshiriki soka la daraja ya kwanza (Sun)

Real Madrid uenda wakaipa klabu ya Spurs kiungo wao wa kati wa Muhispania Isco, 27, na mshambuliaji wa Jamhuri ya Dominica Mariano Diaz, 26, katika juhudi ya kupata saini ya kiungo Eriksen. (El Desmarque - in Spanish)

Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 22, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa kusalia Stamford Bridge baada ya kufunga mabao manane katika ligi ya Premia msimu huu. (Daily Star)

Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa RB Leipzig na Ufaransa wa chini ya miaka-21 Dayot Upamecano, 20, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa Yuro milioni 50. (Mail)

Updated: 22.10.2019 07:00
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.