Tetesi za soka Ulaya Oktoba 7, 2019

Tetesi za soka Ulaya Oktoba 7, 2019

07 October 2019 Monday 06:53
Tetesi za soka Ulaya Oktoba 7, 2019

REAL Madrid wapo tayari kuchuana na Juventus katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante. Vigogo hao wa La Liga wanaweza kulipa dau la uasajili la kufikia pauni milioni 70 ili kumnasa Mfaransa huyo. (Sport, via Mail)

Kocha wa Arsenal Unai Emery anapiga hesabu za kumnunua beki wa Wolves Willy Boly. Wolves wanaweza kutaka dau la pauni milioni 20, wao walimnunua nyota huyo raia wa Ivory Coast kwa pauni milioni 10. (Sun).

Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs anaamini Ole Gunnar Solskjaer anatakiwa kusajili wachezaji wengine watano ili timu irejee kwenye kiwango chake. (Sun)

Makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi baada ya kukubali kichapo cha kushtukiza dhidi ya Newcastle. Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anapigiwa upatu kuchukua mikoba ya Solskjaer. (Sun)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa mrithi wake klabuni hapo atakuwa kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard ama kocha wa zamani wa klabu hiyo, Kenny Dalglish.

Gerrard na Dalgish wote wameichezea Liverpool kwa mafanikio makubwa. (Star)

Beki wa zamani wa Liverpool Glen Johnson amemshauri mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 26, kuihama klabu yake hiyo na ajiunge na Man City. (Manchester Evening News)

Kocha wa Bournemouth Eddie Howe amemtaka mshambuliaji wake Callum Wilson kuzipa kisogo tetesi kuwa Man United inataka kumsajili mwezi Januari. (Daily Echo)

Winga wa Chelsea Christian Pulisic,21, anaripotiwa kutaka kuomba kutolewa kwa mkopo endapo hatopata muda mwingi wa kucheza klabuni hapo. (Sun)

AC Milan walikuwa kwenye mipango ya kutaka kumfuta kazi kocha Marco Giampaolo wakati wa mapumziko wa mechi dhidi ya Genoa siku ya Jumamosi. Mpaka mapumziko Genoa walikuwa wakiongoza kwa goli moja lakini mchezo uliisha kwa Milan kupata ushindi wa 2-1 (SempreMilan, via Star)

Beki wa zamani wa pembeni wa Manchester United Alexander Buttner, 30, amesema alikataa maombi ya usajili kutoka klabu za Uskochi za Celtic na Rangers kabla ya kuamua kutimkia Marekani katika klabu ya New England Revolution. (Goal)

Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Gabriel Agbonlahor, ambaye ndiye mshika rekodi ya kupachika mabao mengi zaidi kwa Villa amefichua kuwa wapinzani wao wa jadi klabu ya Birmingham City walijaribu kumsajili kutoka klabu ya Villa Park wakati alipokuwa mdogo. (Birmingham Live)

Nyota wa zamani wa Liverpool Steve McMahon amemdokeza kocha Jurgen Klopp kumsajili kiungo wa Leicester City James Maddison kabla ya wapinzani wao ahead Manchester United. (Stadium Astro, via Express).

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.