Tetesi za soka Ulaya Septemba 10, 2019

Tetesi za soka Ulaya Septemba 10, 2019

10 September 2019 Tuesday 07:48
Tetesi za soka Ulaya Septemba 10, 2019

BEKI wa Real Madrid,Muhispania Sergio Ramos amemshauri Pogba, 26, kutoka Man United na kuhamia katika klabu yake hiyo Uhispania. (Express)

Chelsea imeanzisha mazungumzo na beki wa Itali Emerson, 25, kuhusu kandarasi mpya.(Sun)

Mlinda lango wa Manchester United David de Gea, 28, anakaribia kutia kandarasi mpya ambayo itampatia mshahara wa paundi 290,000 kwa wiki ikiwa ni mshahaha anaolipwa Pogba. (Guardian)

Winga wa England Callum Hudson Odoi 18 anakaribia kukamilisha mkataba mpya wa malipo ya paundi 180, 000 kwa wiki katika mkataba wa miaka mitano.. (Express)

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi Maurizio Sarri kuzuia uhamisho wa nchezaji huyo wa Brazil. (Mail)

Tottenham iliwatuma wawakilishi ili kumtazama mshambuliaji wa Fenerbahce Vedat Muriqi, 25, akiichezea Kosovo wikendi iliopita.

Maskauti kutoka Lazio, Fiorentina na Napoli pia walikuwepo huku Muriqi akifunga katika ushindi wa Kosovo wa 2-1 dhidi ya Czech Republic. (Sabah, via Four Four Two)

Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen msimu ujao iwapo Paul Pogba ataongeza kandarasi yake na Man United .Eriksen mwenye umri wa miaka 27 atapatikana kwa uhamisho wa bila malipo kwa kuwa kandarasi yake inakamilika 2020. (Sky Sports)

Tottenham ilitaka kumsaini kiungo wa kati wa Roma Nicolo Zaniolo, 20, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo kabla ya kumsaini Giovani lo Celso kwa mkopo badala yake. (Mail)

Chelsea imewambia maajenti wake wakuu kwamba inaamini kwamba marufuku ya uhamisho waliowekewa inayowazuia kununua wachezaji msimu huu itapunguzwa , ikimaanisha kwamba wanaweza kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 27, ametaja baadhi ya ukosoaji dhidi Steve Bruce na klabu hiyo kama upuuzi na aibu. (Chronicle)

Beki Jesus Vallejo, 22, aliyejiunga na Wolves kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la msimu huu anaweza kuuzwa moja kwa moja na klabu yake ya Real Madrid msimu ujao. (Birmingham Mail)

Tamasha kwa jina A Cirque du Soleil kuhusu mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi liitaanza katika mji wa Catalan mwezi Oktoba. (Standard)

Wolves ilishindwa kumsaini kiungo wa kati Leeds Kalvin Phillips msimu huu ,ilibainika baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kusaini mkataba mpya katika klabu yake hiyo.. (Football Insider)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.