Tetesi za soka Ulaya Septemba 16, 2019

Tetesi za soka Ulaya Septemba 16, 2019

16 September 2019 Monday 07:07
Tetesi za soka Ulaya Septemba 16, 2019

BEKI wa zamani wa Man United Gary Neville amesema anaweza 'kukimbia maili moja' iwapo atapewa kazi ya Umeneja Old Trafford. (Manchester Evening News)

Manchester United ilituma mawakala kumchunguza mshambuliaji wa Kosovo, Vedat Muriqi, mwenye umri wa miaka 25, wakati alipofunga dhidi ya timu ya England huko Wembley Jumanne usiku. (Express)

Meneja wa Arsenal, Unai Emery amefichua kwamba alikuwa na Javi Gracia wakati Watford ilipomfuta kazi. (Metro)

Real Madrid na Barcelona zinatarajiwa kushindana kuwania saini ya meneja Jurgen Klopp na mlinzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Liverpool. (AS, kupitia Star)

Manchester United imejipanga kumbakisha  kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, kwa kuhakikisha anakuwa mcheza soka anayelipwa zaidi katika ligi kuu ya England  (Times)

Kiungo Christian Eriksen anapuuzia mkataba mpya anaopendekezewa na Tottenham wakati wakala wa mchezaji huyo mwenye miaka 27 akishughulikia uhamisho kwenda Real Madrid msimu ujao wa joto. (Marca, kupitia Express)

Mchezaji  Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, na kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid, baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chelsea mwenye miaka 28, kuhusishwa na uhamisho kwenda Hispania. (Sun)

Huenda Real Madrid ikamkabidhi mchezaji wa kiungo cha kati Toni Kroos, kwa Manchester United ili kwa upande wake ijipatie mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26, Paul Pogba. (FourFourTwo)

Arsenal inakaribia kufanikiwa kumsajili kijana wa Sunderland Logan Pye baada ya mchezaji huyo wa miaka 15 kuhusishwa ma uhamisho kwenda katika ligi kuu ya England wakati wa msimu wa joto. (Sun)

Kiungo  wa Manchester United, Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, yuko kwenye rada za Juventus . (Mirror)

Updated: 16.09.2019 07:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.