Tetesi za soka Ulaya Septemba 19, 2019

Tetesi za soka Ulaya Septemba 19, 2019

19 September 2019 Thursday 07:22
Tetesi za soka Ulaya Septemba 19, 2019

MASHABIKI wa Real Madrid wakiwa kwenye hasira wametaka kocha wa timu hiyo,Zinedine Zidane afutwe kazi kama meneja wa timu hyo baada ya Paris St-Germain kuitandika kichapo cha mbwa mwizi(3-0) katika mechi ya ligi ya mabingwa (Sun)

Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, anafikiria kustaafu kucheza soka baada ya mashindano ya ubingwa mwaka ujao. (Bild)

Manchester United inatumai itamshawishi kiungo wa timu Paul Pogba mwenye umri wa miaka 26, kusaini mkataba mpya.

Pia Mchezaji Jesse Lingard, mwenye umri wa miaka 26, na mwenzake Mason Greenwood mwenye miaka 17 anayeichezea timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 pia wameorodheshwa kwa ajili ya kupewa mikataba mipya. (Standard)

Juventus ilikataa fursa ya kumsajili beki Dani Alves msimu huu wa joto kabla ya mlinzi huyo mwenye miaka 36 kujiunga na Sao Paulo katika uhamisho wa bure. (Calciomercato)

Manchester United imetuma wakala kwenda kumtazama mchezaji wa timu ya Red Bull Salzburg, raia wa Norway, Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 19, ambaye alifunga magoli matatu kwenye mechi yake ya kwanza katika ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya klabu ya CRG Genk. ( Sport Witness)

Blackburn inafanya mazungumzo kumsajili aliyekuwa kiungo wa Tottenham na Fulham Lewis Holtby, raia huyo wa Ujerumani mwenye miaka 29 ambaye amekuwa wakala tangu aondoke Hamburg msimu uliopita. (Mail)

Everton ina hamu ya kumsajili mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 wa Ireland kaskazini David Parkhouse, ambaye kwa sasa amechukuliwa kwa mkopo na Derry City kutoka Sheffield United. (Football Insider)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.