Tetesi za soka Ulaya Septemba 20, 2019

Tetesi za soka Ulaya Septemba 20, 2019

20 September 2019 Friday 06:49
Tetesi za soka Ulaya Septemba 20, 2019

KLABU ya Liverpool imeanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba wa miaka mitano na nusu mshambuliaji wake rai wa Senegal Sadio Mane, 27. Mkataba huo utamfanya Mane awe mchezaji anayelipwa vizuri zaidi Anfield kwa kitita cha pauni 220,000 kwa wiki. (Gazzetta dello Sport kupitia Star)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku na mchezaji mwenza Marcelo Brozovic ilibidi waamuliwe na Alexis Sanchez baada ya kuibuka tafrani kwenye chumba cha kubadili nguo baada sare ya 1-1 Slavia Prague siku ya Jumanne. (Mail)

Kiungo wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 27, amesema anahisi "kutokuwa na furaha kidogo" kwa kupata muda mdogo wa kucheza klabuni Liverpool msimu huu japo anasisitiza kuwa yungali na "furaha" kuwa Anfield. (Liverpool Echo)

Klabu ya Real Madrid itawapasa watoe kitita cha euro milioni 80 wakitaka kumfuta kazi kocha wao Zinedine Zidane. Zidane amekuwa kwenye shinikizo kubwa kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri. (Sport)

Barcelona sasa ni klabu kubwa nyengine inayotajwa kumnyemelea mshambuliaji kinda Erling Braut Haaland, 19, wa klabu ya Red Bull Salzburg. Raia huyo wa Norway alikuwa mwiba mkali kwa klabu ya KRC Genk (inayochezewa na Mtanzania Mbwana Samatta) kwa kufumania nyavu zao mara tatu siku ya Jumanne. (Mundo Deportivo)

Baba wa Haaland, Alf-Inge, ameweka wazi kuwa itakuwa "vizuri" endapo mwanawe atajiunga na Manchester United, licha ya baba mtu kuchezea klabu hasimu za Leeds na Manchester City katika enzi zake. (TV2 kupitia Mail)

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania David Silva, 33, anatarajiwa kujiunga na klabu inayomilikiwa na David Beckham Inter Miami ya nchini Marekani pindi tu mkataba wake na Man City utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu. (Independent)

Mmiliki wa klabu ya Arsenal Stan Kroenke alitoa pesa yake mfukoni kusajili wachezaji katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi badala ya kutegemea pesa kutoka kwenye vyanzo vya klabu kama inavyoinishwa kwenye sera zao.(Mirror)

Chelsea wana Imani kuwa majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata kiungo wao Mason Mount, 20, kwenye mchezo dhidi ya Valencia siku ya Jumanne si makubwa kama ilivyohofiwa hapo awali. (Standard)

Leicester wametuma maskauti wao kumtazama beki wa pembeni wa Benfica, Mreno Andre Almeida, 29, kwenye mchezo dhidi ya RB Leipzig siku ya Jumanne. (Record kupitia Leicester Mercury)

Everton na Newcastle wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa Atlanta United na Venezuela Martinez, 25. (Chronicle)

Kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 24, anaamini kuwa anaweza kuchezea timu ya taifa ya England baada ya kupewa maneno ya hamasa na kocha msaidiza wa Villa, John Terry. (Standard)

Updated: 20.09.2019 06:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.