banner68

Tetesi za Usajili: Juuko Murshid ‘out’ Simba

Simba yapata mbadala wake aliyekuwa anacheza soka la kulipwa Ulaya

Tetesi za Usajili: Juuko Murshid ‘out’ Simba

Simba yapata mbadala wake aliyekuwa anacheza soka la kulipwa Ulaya

21 June 2018 Thursday 11:39
Tetesi za Usajili: Juuko Murshid ‘out’ Simba

Na Amini Nyaungo

Wakati Simba ikijiandaa kuachana na beki wao Mganda Juuko Murshid, vigogo wa kamati ya usajili wa timu hiyo wamepata mbadala wake kutoka nchini Kenya.

Simba inaelekeza nguvu zake nje ya nchi kwa aina ya usajili ambao wanahitaji kuufanya hasa baada ya kupewa chachandu ya muwekezaji mkuu wa timu hiyo Mohamedi Dewji naye akiwa ndani ya kamati ya usajili.

Yupi mbadala wa Juuko Murshid?

Mussa Mohamed nyota wa zamani wa Gor Mahia ambaye alitimka mwezi Januari kuelekea nchini Albania katika klabu ya KF Tirana inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Simba inajiandaa na maisha bila ya Juuko ambaye hata hivyo hakuwa anapata nafasi mara kwa mara ndani ya Wekundu wa Msimbazi.

Habari za uhakika zinasema nyota huyo Mussa Mohamed hawezi kuruka kwani kwa sasa yupo huru kwani amemaliza mkataba wake na klabu ya Tirana hivyo atasaini Simba.

Inawezekana ikawa jina geni katika masikio ya wengi lakini ni moja ya mabeki wazuri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ambao ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo endapo watamsajili.

Juuko Murshid `out`

Beki huyo ambaye anakiwango cha hali ya juu huku akiwa kipenzi cha mashabiki na wanachama wa Simha hakuwa na wakati mzuri tangu asajiliwe kikosini hapo.

Hakuwa anatumika sana kutokana na mahitaji ya mwalimu na amekuwa na bahati mbaya walimu wote waliopita hawakuwa wanamtumia.

Azania Post

Updated: 21.06.2018 14:36
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.