Tetesi za usajili: Kipre Tchetche kurejeshwa Azam

Tetesi za usajili: Kipre Tchetche kurejeshwa Azam

29 May 2018 Tuesday 11:25
Tetesi za usajili: Kipre Tchetche kurejeshwa Azam

Na Amini Nyaungo

Timu ya soka ya Azam inatarajia kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji hatari wa timu hiyo na raia wa Ivory Coast Kipre Tchetche ambaye alitimkia Ulaya misimu miwili iliyopita.

Tchetche ambaye anacheza Terengganu F.C. ya Kuala Luampa Malaysia anatarajia kurejea kwa mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania Bara.

Aidha habari za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zinasema ujio wa mchezaji huyo utaleta chachu katika safi ya ushambuliaji.

Wakati huo huo Azam wanahitaji saini ya Tafadzwa Kutinyu wa Singida United wakati washatwaa saini ya Donald Ngoma kutoka Yanga huku kocha Hans Van Pluijm umekuwa na harakati nyingi za kuweza kuirudisha timu hiyo katika ubora wake.

Wachezaji wengine ambao wanatakiwa katika kikosi cha Azam ni pamoja na Deus Kaseke, Mudathir Yahya pamoja na kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko.

Azam waliwahi kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2012-2013 kocha akiwa Stewart Hall raia wa Uingereza.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.