Tetesi za Usajili: Obrey Chirwa afichwa, kutua Msimbazi

Yanga hawajui alipo, vyanzo ndani ya Simba vinasema wanataka aongeze nguvu safu ya ushambuliaji

Tetesi za Usajili: Obrey Chirwa afichwa, kutua Msimbazi

Yanga hawajui alipo, vyanzo ndani ya Simba vinasema wanataka aongeze nguvu safu ya ushambuliaji

18 June 2018 Monday 11:05
Tetesi za Usajili: Obrey Chirwa afichwa, kutua Msimbazi

Na Amini Nyaungo

Wakati Obrey Chirwa ametimka Yanga, wiki iliyopita mchezaji huyo ameonekana yupo Misri kupitia mitandao ya kijamii, huku baadhi ya magazeti hapa nchini na Radio zilisema mchezaji huyo huenda atasaini klabu moja huko Misri lakini bado kuna kitendawili hakijateguliwa.

Mchongo uko hivi

Azania Post imemtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Yanga Hussein Nyika, amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo ameondoka, ila hata wao wanaona katika mitandao yupo nchini Misri ila hawajui kuwa yupo wapi.

Wanasubiri taarifa ilimradi wafanye maamuzi mengine ya kuongeza wachezaji wapya maana bado wachezaji 3 wa kigeni.

Tetesi mpya za usajili zinasema kuwa Chirwa amefichwa na kamati ya usajili ya wataji wa jadi Simba ‘Msimbazi’ huku wakisubiri muda kumtangaza.

Simba bado wanahitaji kuongeza wachezaji watakaoisadia timu kuelekea kwenye michuano ya kimataifa, kwa taarifa ya msemaji mkuu wa timu hiyo Haji Manara amesema kuwa wanaweza kusajili mchezaji yoyote kutoka nchi za Afrika.

Chanzo chetu kinasema Chirwa alishazungunza na kamati ya usajili ya Simba inayoongozwa na Hans Pope msimu ujao atavaa jezi yenye rangi nyekundu na kijani.

Simba ndio mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara wamefungwa mchezo mmoja katika michezo 30 ya msimu uliopita huku ikifunga Zaidi ya magoli 60 na kufungwa 14.

Azania Post

Updated: 18.06.2018 11:08
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
elifarig 2018-06-26 14:37:00

big up kwao