Tetesi za usajili: Said Ndemla kupewa jezi namba 8 Yanga

Tetesi za usajili: Said Ndemla kupewa jezi namba 8 Yanga

17 June 2018 Sunday 11:46
Tetesi za usajili: Said Ndemla kupewa jezi namba 8 Yanga

Na Amini Nyaungo

Jezi namba nane ambayo Maka Edward wa Yanga ametangaza kuiacha msimu ujao huku akisema inamtu maalumu, inanukia kupata mwenyewe, na habari zake zitatangazwa muda si mrefu.

Said Hamis Ndemla, moja ya wachezaji mahiri ambao wamesakwa na Yanga kwa muda mrefu, huenda msimu ulioisha kama si Mkude basi Ndemla angemfuata Ajibu.

Sasa mambo yanaonekana kuwa tayari, na habari za kuaminika zinasema Ndemla ameomba ruhusa kwa Simba kuwa wamuachie aende akasaini Jangwani.

Tatizo kubwa sio kuikataa Simba bali anakosa nafasi ya kuitumikia klabu hiyo kutokana na wingi wa wachezaji wanaocheza katika nafasi yake ya kiungo kwa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara Simba.

Lakini pia tatizo lipo kwa kocha Masudi Djuma ambaye anaonekana kutokuwa tayari kumwona kiungo huyo mahiri anaachana na Simba akifanya kila liwezekanalo ili aendelee kubaki huku akimuahidi kumpa nafasi zaidi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao endapo atapewa yeye jukumu la kuinoa Simba kama kocha mkuu.

Habari zinasema Ndemla ameitikia wito huo lakini bado anafikiria endapo Simba wakimsaini kocha mwingine inamaana ahadi hiyo itapotea na kushindwa kutimiza ndoto yake ya kusakata kabumbu na kuonesha kile alichojaaliwa.

Msemaji mkuu wa Simba Haji Manara amekanusha tetesi hizo licha ya kukubali kuwa Ndemla mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu wakati mwingine anakosa bahati ya kucheza.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
jonh 2018-06-17 23:45:02

0767546211

Avatar
LAMECK DAUD 2018-07-06 10:21:08

SIMBA MUACHIENI NDEMLA AJIENDEE JANGWANI KWANI KUMUWEKA KAMA MZIGO MTAMFANYA APOTEZE KIWANGO CHAKE KWANI ANAKIPAJI, MUACHENI AONDOKE

Avatar
Godifrey Jackson 2018-07-06 12:01:52

Ndemla Bwana Hata Kama N Mazngra Unaweza Kubadilisha Na Kuhama Kwenda Klabu Nyngne.

Avatar
fedrick karumani 2018-07-09 21:50:01

simba mwachen aende kutafuta kwan rizk nipopote

Avatar
Double J 2018-07-10 14:13:53

Ni sawa anachozungumza demla but aangalie na timu ya kwenda acje kubomoa akidhani ndo kujenga

Avatar
Emma C Msuka 2018-07-12 09:44:35

Mpeni Ruhusa Aje Yanga Sisi 2ko Tayari Kumpokea

Avatar
Ismail matimba 2018-07-12 13:27:53

M ningependa tuachane mambo ya kusajili wachezaji Loyola simba wengi wao hawafanyi vizuri, mfano mzr okwi kaseja walikua mamluki tu.

Avatar
Ismail matimba 2018-07-12 13:36:53

M ningependa tuachane mambo ya kusajili wachezaji Loyola simba wengi wao hawafanyi vizuri, mfano mzr okwi kaseja walikua mamluki tu.