Tetesi za Usajili: Simba bado, wamgeukia Hassan Dilunga

Ni baada ya Yanga kusuasua katika kuoata saini yake

Tetesi za Usajili: Simba bado, wamgeukia Hassan Dilunga

Ni baada ya Yanga kusuasua katika kuoata saini yake

03 July 2018 Tuesday 19:04
Tetesi za Usajili: Simba bado, wamgeukia Hassan Dilunga

Wakati sekeseke la usajili hapa Tanzania likizidi kushika kasi kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, imeelezwa mabosi wa Simba tayari wameshamalizan na kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema kuwa Kamati ya Usajili imeshamaliza kufanya mazungumzo na Dilunga na kufikia makubaliano na kilichobaki ni kupewa mkataba wa kusaini.

Dilunga ameelezwa kumalizana na Simba ikiwa ni siku kadhaa zilizopita iliripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na timu yake ya zamani ya Yanga lakini inaonekana wameanza kupigwa kete na watani zao wa jadi Simba.

Simba wameanza harakati za kuanza kuimarisha zaidi eneo la kiungo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano ya kimataifa ya CAF ambapo itakuwa inaiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika kikao kilichoitishwa mara ya mwisho mbele ya waandishi wa habari, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, alifunguka na kusema Kamati ya Usajili itaendelea kufanya usajili kulingana na mapendekezo ya Kocha.

Hatua hii waliyofika nayo Simba kwa Dilunga, unakuwa unawapa wakati mgumu watani zao wa jadi Yanga ambao nao wanawania saini yake, kutokana na jeuri ya fedha za Mohamed Dewji kwa wekundu hao wa Msimbazi.

Updated: 03.07.2018 19:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.