Tetesi za usajili: Simba kumsajili Deus Kaseke

Pia Azam FC inamnyatia mchezaji huyo wa Singida United

Tetesi za usajili: Simba kumsajili Deus Kaseke

Pia Azam FC inamnyatia mchezaji huyo wa Singida United

12 June 2018 Tuesday 14:04
Tetesi za usajili: Simba kumsajili Deus Kaseke

Na Amini Nyaungo

Habari za usajili kwa klabu ya Simba zinazidi kushamiri huku ikidaiwa kwamba winga mahiri wa Singida United Deus Kaseke huenda akawa mbioni kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ajili ya msimu ujao.

Huenda ikawa habari ngeni kwa mchezaji huyu kujiunga na klabu hiyo ya Msimbazi ila ndio hivyo tena kocha amependekeza asajiliwe.

Inaelezwa kuwa kocha ambaye haijulikani hatma yake kama ataondoka au atabaki, Pierre Lichantree amelipeleka jina la nyota wa zamani wa Yanga, Deus Kaseke pamoja na beki wa Singida United Kenedy Juma kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Kaseke ambaye alikuwa na dili la kusakata kabumbu Afrika Kusini, dili hilo limeota mbawa mara baada ya moja ya timnu ambazo alitarajiwa kujiunga kuweka sharti kwamba awe ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania.

Hivyo endapo Simba watahitaji huduma ya mchezaji huyo mlango uko wazi.

Pia Azam wanaonekana kukaa mkao wa kula kuweza kumnasa mchezaji huyo mara baada ya Hans Van Pluijm kuonekana kuhitaji watu aliofanya nao kazi Singida na Yanga.

Ni sahihi kwa mchezaji huyo kusajiliwa na Simba, timu ambayo msimu ujayo itakuwa inakabiliwa na mashindano makubwa barani Afrika hivyo kuhitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa zaidi?

Jiunge katika mjadala wetu kupita facebook, Instagram na Twitter tuambie unaonaje.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Samweli Petro shunashu 2018-06-12 19:24:34

Ajeatatu saisia

Avatar
khalid shaban kabendua 2018-06-13 11:42:42

me naon ap saw kasek azame msimbaz au vp

Avatar
Man simba 2018-06-25 15:36:19

Kaseke anatisha sana Msimbazi ndo maala pake karibu xana kaseke ule bata na Mo Dewij.

Avatar
Bakari nassor 2018-07-01 08:51:11

Kaseke njoo msimbazi kwenye kisima cha kuchimba pesa

Avatar
Doto Amani 2018-07-02 17:39:14

Kaseke Njoo Kwenye Raha Bila Kifo

Avatar
Godifrey Jackson 2018-07-06 11:54:54

Kaseke Njo Uone Uhondo Wa Soka Simba Pamoja Na Raha Tupu.

Avatar
Lameck aron 2018-07-07 08:32:15

Kaseke hiyo bahati pia kuhitajika msimbazi kama vp changamkia frusa njoo uone raha ya magori msimbaz pamoja na kla bata kwa xana

Avatar
0787161014 2018-07-12 17:51:57

KASEKERAHAYANGASIMBASHIDATU