Tetesi za Usajili: Simba kushusha nyota wakali wawili wakigeni,

Simba pia wamepanga kuzungumza na kocha Lichantree kumshawishi kusaini mkataba mwingine

Tetesi za Usajili: Simba kushusha nyota wakali wawili wakigeni,

Simba pia wamepanga kuzungumza na kocha Lichantree kumshawishi kusaini mkataba mwingine

19 June 2018 Tuesday 11:29
Tetesi za Usajili: Simba kushusha nyota wakali wawili wakigeni,

Na Amini Nyaungo

Simba inatarajia kushusha wachezaji wawili wa kigeni huku ikimalizia kusaini mikataba ya wachezaji wake waliomaliza mikataba.

Kauli hiyo imethibitishwa na Msemaji Mkuu wa timu hiyo Haji Manara, kuwa wanataka kutengeneza kikosi imara kitakachokuwa kina ushindani wa hali ya juu.

“Tupo tayari kwa mapambano, kwa sasa tunashughulikia wachezaji waliomaliza mikataba yao, wakati huo huo tunahitaji kuongeza wachezaji nyota wawili wakubwa kutoka nje ambao wataungana na wenzao wa Simba,” amesema.

Manara pia amesema kuwa uhasimu wao dhidi ya Yanga ni uwanjani, amewaomba wasajili vizuri ili walete ushindani, amekumbushia kuwa huu ndio muda wao wa kukaa benchi kama walivyokaa wao kipindi cha nyuma.

“Yanga ni mahasimu wetu uwanjani tu, wajitahidi wachague wachezaji wazuri ili kuwe na ushindani, sisi ndio tayari tumeshajiaanda vizuri,” amesema.

Katika sakata lingine amesema kuwa wanajaribu kuongea na Lichantree kama ataweza kusaini mkataba mpya au watafute kocha mwingine.

Kwa kauli yake inaonesha dhahiri kabisa ripoti zilizopita za kutoendelea naye kwa kocha huyo, hivi sasa wanajiandaa na kocha mwingine.

Simba wanajiandaa na michuano ya Kagame Cup pamoja na ile ya kimataifa msimu ujao.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
xupa 2019-06-07 07:49:17

simba hana aibu na hali ya yanga maana tunaona yanga kujifananisha na timu za sodo mitaan aseme ivyo yanga nivibonde

Avatar
mudi okono 2019-06-20 22:22:34

manara achana nayanga amnawachezaji apo kama vipi wafuejezi poa

Avatar
mudi okono 2019-06-20 22:25:28

manara achana nayanga amnawachezajiapo kamavipi wafuejez poa

Avatar
xheby 2019-06-27 02:34:47

kweli yanga hawana lolote lakuwatixhia ximba

Avatar
Rajabu ezra 2019-06-27 22:51:15

Ongeleni simba tunaombo mfanye usajili utakoo tufikishi kwenye malengo mazri.asanteni sana.ukhwa na simba hakuna kuogopa.

Avatar
joshua 2019-07-03 13:23:25

manara this is simba, tunaomba usajir uwe wa uhakika, wenye malengo,

Avatar
yona kirasi nnko 2019-07-04 20:43:12

ki2nitakacho omba uyo kocha aondoke ana mbinu ya aina yeyote tafuteni kocha

Avatar
mr fazo 2019-07-05 17:14:29

2naxajir kwaajr yakimataif co bongo land