Tetesi za usajili: Simba wahamia kwa ‘Ninja’

Tetesi za usajili: Simba wahamia kwa ‘Ninja’

31 May 2018 Thursday 12:11
Tetesi za usajili: Simba wahamia kwa ‘Ninja’

Na Amini Nyaungo

Mambo ni moto katika harakati za usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu hapa Tanzania Bara.

Azam FC tayari wamemtaja Hans Van Pluijm kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja kwa Singida United.

Wakati huohuo Singida United wameifanya umafia Yanga baada ya kumsajili Tiber John, ambaye alikuwa akitokea Mtwara kuja jijini Dar es Salaam kujiunga na Yanga, lakini alinyakuliwa maeneo ya Temeke na wakali hao wa Singida na kumtoa mikononi mwa vijana wa Jangwani.

Simba

Simba bado wanaendelea na harakati zao za kulipa kisasi kwa kupitia usajili wa wachezaji mahiri kutoka kwa mahasimu wao wa jadi, na sasa inadaiwa kuhamia kwa mlinzi wa mabingwa mara 27 Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ili kuchukua nafasi ya Juuko Murhid ambaye inadaiwa kuwa anatemwa katika kikosi hiko.

Huku Laudit Mavugo naye anakaribia kuachwa baada ya msaada wake katika timu hiyo kuonekana kupungua, kinyume na matarajio ya klabu hiyo wakati wakimsajili.

Yanga

Mchezaji wao wa zamani Mrisho Ngassa taarifa rasmi zinasema amesajiliwa na timu hiyo. Hii inatokana na mapenzi ya mchezaji huyo.

Viongozi wa Yanga bado hawajaweka usajili wa Ngasa hadharani, ila taarifa sahihi zinasema tayari amekwishatia saini kuichezea klabu hiyo ya Jangwani kwa msimu ujao wa ligi kuu Bara.

Jezi namba 8 ya Yanga ambayo alikuwa anatumia Maka Edward ameiacha rasmi huku mchezaji huyu akisema anampa mchezaji aliyesajiliwa hivi karibuni, hivyo kuna mchezaji amesajiliwa na atatambulishwa.

Singida United

Singida United wamefanya umafia Yanga baada ya kumpora kinda mwenye kipaji cha hali ya juu Tiber John na inaelezwa atatangazwa muda si mrefu na klabu hiyo.

Huku kuna mchezaji kutoka Amerika naye ametua katika timu hiyo na leo mchana watatangaza usajili wote.

Azam

Waoka mikate wa Azam wamemtambulisha kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van Pluijm kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, amechukua mikoba ya Aristica Ciaoba.

Juma Abdul imetaarifiwa kuwa anajiunga na Azam baada ya hapo jana kusambaa taarifa lukuki za mchezaji huyo kuelekea huko na katika safari ya wachezaji walioenda Kenya hayupo.

Azania Post

Updated: 31.05.2018 12:29
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.