Tetesi za usajili: Simba yahamishia majeshi kwa Obrey Chirwa

Baada ya mbio za kuwanyakua Tshishimbi na Yondani kukwama, Simba yahamia kwa Obrey Chirwa

Tetesi za usajili: Simba yahamishia majeshi kwa Obrey Chirwa

Baada ya mbio za kuwanyakua Tshishimbi na Yondani kukwama, Simba yahamia kwa Obrey Chirwa

07 June 2018 Thursday 12:41
Tetesi za usajili: Simba yahamishia majeshi kwa Obrey Chirwa

Na Amini Nyaungo

Kama ulikuwa unadhani kuwa Simba wamesitisha harakati zao za kuibomoa Yanga kwa kuchukua baadhi ya nyota wake utakuwa ulikosea maana sakata hilo linaendelea na zile tetesi za Mzambia Obrey Cholla Chirwa kutakiwa na wekundu wa Msimbazi zina ukweli ndani yake.

Taarifa ambazo Azania Post imezipata wakati Uongozi wa Yanga ukihangaika kumpa mkataba mpya nyota huyo, Simba wamejitoa mhanga na kumuahidi donge nono Mzambia huyu ambaye hutumia nguvu na kujituma uwanjani.

Simba ambayo ina jeuri ya pesa msimu huu baada ya mambo kuwakalia sawa, wanatesa katika jukwaa la usajiri huku wakitanabaisha kuwa wanauwezo wa kumchukua mchezaji yoyote kutoka timu yoyote ya ligi kuu bara.

Awali walikuwa wanataka kumsajili Papy Tshishimbi Yanga wakashtukia wakamuwahi, wakataka kumsajili beki Kevin Yondani Yanga wakashtukia dili, sasa wanahitaji kumchukua mshambuliaji mahiri Chirwa, na huenda wakafanikiwa.

Chirwa msimu wake wa pili huu akiwa amefunga magoli 24 ligi kuu Tanzania bara kwa misimu miwili huku akifunga magoli 6 ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.