Tetesi za usajili: Simba yaifumua Yanga, Tshishimbi ndani ya uzi mwekundu

Tetesi za usajili: Simba yaifumua Yanga, Tshishimbi ndani ya uzi mwekundu

29 May 2018 Tuesday 13:41
Tetesi za usajili: Simba yaifumua Yanga, Tshishimbi ndani ya uzi mwekundu

Na Amini Nyaungo

Kuna tetesi zimeanza kuzagaa kwamba nyota wa Yanga Papy Tshishimbi yupo mbioni kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ajiri ya kuitumikia klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi.

Tshishimbi ambaye anacheza nafasi ya kiungo mkabaji imeelezwa tayari amemalizana na Wekundu wa Msimbazi na usajili wake utatangazwa kabla ya kuelekea katika michuano ya SportsPesa Super Cup, ambayo yatafanyika nchini Kenya.

Msemaji wa Simba Haji Manara alinukuliwa akisema kwamba Simba italipa kisasi kwa waliowahi kuwanyanyasa hapo zamani, na huenda kisasi hicho kinaelezwa Yanga.

"Tunalipa kisasi, tutatangaza habari nyingine kubwa kabla ya kuelekea Nairobi," amesema.

Papy Tshishimbi bado ana mkataba wa mwaka mmoja umebakia na kuvunja mkataba huo inaonekana sio tatizo kwa Simba chini ya tajiri Mohamed Dewji.

Simba tayari imefanya usajili wa wachezaji wawili Marcel Kaheza na Adam Salamba.

Azania Post

Updated: 29.05.2018 15:02
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
i,naldo 2018-06-28 21:44:19

naiomba simba imsajili shishimbi

Avatar
alphanation 2018-07-12 23:51:34

mbwembwe2 hamna lolte

Avatar
Mr Mkicha 2018-07-17 20:40:00

Mimi ni shabikh wa Simba ila kwa usajili wa Wawa--kwetu ni mzigo.Why uongozi usimsajili YONDANI?

Avatar
Exsevia Nicholaus Sekelo 2018-05-31 08:19:38

simba hii ni on fire

Avatar
juma 2018-06-26 13:33:20

748643

Avatar
Anaph 2018-07-10 14:41:47

SIMBA DAMU; NAOMBA SEHEM YA KIUNGO ISIHALIBU AKUNA TATIZO, ILA BEK NA 4WAD

Avatar
ISIHAKA HARUNA MAHUBA KUTOKA KIGOMA 2018-07-17 17:19:20

SIMBA SPORT CLUB kaa mbalinayo

Avatar
Fuluku Fuluku 2018-07-21 23:10:27

Simba Yondan Muhujumt Mchukue Ali Ali Kutoka Stend