banner68
banner58

Tetesi za Usajili: Watakaoongezwa Simba wakati wa dirisha dogo la usajili watajwa

Tetesi za Usajili: Watakaoongezwa Simba wakati wa dirisha dogo la usajili watajwa

03 November 2018 Saturday 09:26
Tetesi za Usajili: Watakaoongezwa Simba wakati wa dirisha dogo la usajili watajwa

Wakati ikielezwa kuwa mabosi wa klabu ya Simba wapo kwenye mchakato wa kuachana na baadhi ya wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kuonesha viwango vyao, inaelezwa pia mabosi hao wapo kwenye mkakati wa kushusha vyuma vingine katika usajili wa dirisha dogo.

Wachezaji ambao wanapigiwa upatu hivi sasa ni jina la Salum Kimenya ambaye anakipiga Tanzania Prisons ya Mbeya ambaye atatua kuchukua nafasi ya Mohammed Rashid.

Aidha, jina la kiungo Francis Kahata wa Gor Mahia FC nalo limekuwa likihusishwa zaidi tangu kumalizika kwa msimu uliopita kuna uwezekano kiungo huyo akajiunga na Simba dirisha dogo.

Ukiachana na Kahata, mipango hiyo ambayo Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ndiye mpikaji wa kila kitu, inaelezwa amependekeza usajili huo ufanyike ili kukifanya kikosi chake kuwa imara zaidi.

Aussems ana imani kikosi cha Simba kikikamilisha suala hilo kinaweza kufanya vema zaidi pia katika mashindano ya mechi za kimataifa ambazo zinakuja hivi karibuni.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Khashil Athuman 2018-11-08 14:28:30

Simba Sc Wakawaka.