banner68

Tetesi za usajili: Yanga kukamilisha usajili wa mkali wa Gor Mahia

Alikuwa ni mfungaji bora wa michuano ya SportsPesa Super Cup iliyomalizika hivi karibuni

Tetesi za usajili: Yanga kukamilisha usajili wa mkali wa Gor Mahia

Alikuwa ni mfungaji bora wa michuano ya SportsPesa Super Cup iliyomalizika hivi karibuni

13 June 2018 Wednesday 11:46
Tetesi za usajili: Yanga kukamilisha usajili wa mkali wa Gor Mahia

Na Amini Nyaungo

Yanga wako mbioni kumsajili kiboko ya Simba Meddie Kagere wa Gor Mahia ambaye ndiye mfungaji bora wa michuano ya SportsPesa Super Cup yaliyomalizika Juni 10.

Azania Post ilitaka kupata ukweli juu ya uvumi huu na ikaongea na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amekiri kuwa Kagere ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kuisaidia Yanga, kuelekea michuano ya kimataifa.

"Ni kweli tunataka mchezaji wa kimataifa aweze kuungana na wenzake hapa Yanga, kwa Kagere moja ya washambuliaji hatari, inawezekana ikawa hivyo ila bado," amesema.

Kagere tayari amefikisha miaka 31, hivyo iwapo Yanga watakamilisha usajili wake, huenda watafaidika naye msimu mmoja au miwili tu.

Tatizo la umaliziaji kwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara limekuwa tatizo kubwa kutokana na washambuliaji wake kuwa majeruhi wa muda mrefu, huku wengine wakigoma kucheza kutokana na ukata ambao umeiathiri timu hiyo.

Azania Post

Updated: 13.06.2018 11:50
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
makoyebukela 2018-06-16 16:41:25

Yanga Fanya usajiri wa maana sio kuzoazoa kama akina ajib anaecheza na jukwa na kupoza Moira watu wakiwa kwenye muvu

Avatar
NYEHA LYANKONO 2018-06-18 21:57:31

subirin tuwaandalie dawa zenu wanasimba mtakimbia kagere ,chirwa,ajbu kat tshitshimbi nawaamin watarejesha heshma ya yanga tena daima

Avatar
Godifrey Jackson 2018-07-06 12:07:50

Hakika Yanga Inakufa Msimu Ujao Tena

Avatar
makoyebukela 2018-06-16 16:44:40

Yanga Fanya usajiri wa maana sio kuzoazoa kama akina ajib anaecheza na jukwa na kupoza Moira watu wakiwa kwenye muvu

Avatar
mrope junior 2018-06-18 13:59:20

kwa hakika mmekosa jipya msimu huu

Avatar
Mzee wa suna 2018-06-18 17:23:55

Fanyeni usajili wa maana kwami mmekua mnatuvunja nguvu wenzetu pindi yanapotokea matokeo mabovu

Avatar
Johh baraza 2018-06-19 09:16:24

Yanga fanyen uxajil wa maan achen kubabaixha fanyen mzaha mtaibika mxim ujao kwa wapinzan wen

Avatar
Eligius Kapinga 2018-06-19 22:00:07

Yanga Fanyeni Usajili Wa Kwel Tuludishe Nguvuzetu Msim Ujao