Tetesi za Usajili: Yanga yaifanyia umafia Simba

Tetesi za Usajili: Yanga yaifanyia umafia Simba

15 June 2018 Friday 16:51
Tetesi za Usajili: Yanga yaifanyia umafia Simba

Na Habakuki Urio,

Hata Kama Hutaki kusikia hii, habari ndo hiyo! Yanga wameshafikia makubaliano ya mwisho na mshambuliaji hatari, kiboko ya Simba Meddie Kagere kutoka Gor Mahia na muda wowote anatamwaga wino Jangwani.

Taarifa za uhakika kutoka katika Kamati maalumu ya marekebisho ya klabu ya Yanga iliyo chini ya Abbas Tarimba zinasema kuwa mbali na mshambuliaji huyo kamati hiyo itashusha majembe mengine ya kutosha na kushutua akili za watu wengi.

“Ni kweli tupo kwenye hatua za mwisho na mara baada ya kila kitu kuwa pouwa tutaweka mambo yote hadharani. Wanayanga watulie kilakitu kitakuwa sawa na watafurahi kwa msimu ujao,” alisema moja ya mjumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo taarifa Zaidi zinasema Yanga inataka kufanya umafia kwa kumsajili kiungo Fransic Kahata ambaye amekuwa kwenye mazungumzo ya karibu na Simba kwa siku za hivi karibuni.

Azania Post

Updated: 16.06.2018 12:52
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
issa ngoya 2018-06-15 21:18:50

"jamani wana yanga mbona tupo wengi tz tuwasaidie kamat ya usajili hata kwa michango yetu mbona tunazidi kuchekwa"

Avatar
Sahani jb jr 2018-07-12 22:19:02

Usajil wa kimya kimya lengo ni nin?

Avatar
joseph simon 2018-07-14 09:14:29

jamani wanayanga tunahitaji mabadiliko ili klabu yetu izidi kusonga mbele pia kuwa na umoja na mshikamano tuisapoti timu yetu kwa kuishangilia hii itasaidia wachezaji kuwa na molali na kujituma .Yanga daima mbele nyuma mwiko.