TFF, Azam Media wasaini mkataba bilioni 4.5

TFF, Azam Media wasaini mkataba bilioni 4.5

12 September 2019 Thursday 16:48
TFF, Azam Media wasaini mkataba bilioni 4.5

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

SHIRIKISHO la soka nchini(TFF) limesaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Azam Media kuonesha moja kwa moja mechi za timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mkataba wa awali wa Azam Sports umefikia tamati msimu uliopita na sasa pande hizo zimesaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya bilioni 4.5

Pia mkataba wa kuonesha mechi za Taifa Stars umegharimu milioni 400 ambazo ni sawa milioni 100 kwa mwaka, na kwenye kila mechi Taifa Stars itapata milioni 35 kutoka Azam Media.

Akitoa ufafanuzi wa mkataba huo Mkurugenzi wa Michezo wa Azam Media Patrick Kahemele amesema mechi za Taifa Stars zilizodhamini na Azam ni zile za kirafiki zitakazokuwa kwenye kalenda ya FIFA.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.