banner68
banner58

TFF yaipongeza Yanga kusonga mbele kimataifa

Yanga imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi

TFF yaipongeza Yanga kusonga mbele kimataifa

Yanga imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi

19 April 2018 Thursday 17:15
TFF yaipongeza Yanga kusonga mbele kimataifa

Na Habakuki Urio

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia ameipongeza klabu ya Yanga kwa kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Africa.

Yanga imefanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza kwa mabao 2-0 kabla ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Welaitta Dicha ya Ethiopia.

Rais wa TFF Ndugu Karia kwa niaba ya TFF ameipongeza klabu ya Young Africans kwa hatua hiyo kubwa iliyofikia ambayo inaakisi mpira wa Tanzania kiujumla.

“Mafanikio ya klabu ya Young Africans ni mafanikio ya Tanzania kiujumla na TFF ambao ni wasimamizi wa mpira nchini tunajivunia mafanikio hayo ya Young Africans ambao tumekuwa tunashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Tanzania,” amesema Karia.

Amesema anaamini watafanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye hatua hiyo ya makundi.

Azania Post

Updated: 19.04.2018 18:30
Keywords:
TFFYanga
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
hashim salehe 2018-04-20 13:34:19

Mimi kama shabiki wa kweli wa yanga African nasema ahsante ni kwa kuipa sapot timu ya yanga na mungu awabariki sana.