TFF yamfungashia virago Amunike

TFF yamfungashia virago Amunike

08 July 2019 Monday 19:47
TFF yamfungashia virago Amunike

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

SHIRIKISHO la soka nchini(TFF) limemfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, ikiwa ni siku chache zimepita baada ya timu hiyo kutolewa hatua ya makundi kwenye fainali za AFCON.

Taarifa iliyotolewa ya TFF leo Julai 8, 2019 imeeleza kuwa pande mbili zimefikia makubaliano ya kusitisha mkataba huo.

''Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Emmanuel Amunike tumefikia makubaliano ya pamoja kusitisha mkataba baina yetu''.

Aidha TFF imeweka wazi kuwa itatangaza kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.

Pia immefafanua zaidi kuwa makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019.

Kwasasa shirikisho limebainisha kuwa mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja.

TFF itatangaza Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.

Updated: 11.07.2019 21:11
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.