banner68

TFF yatoa onyo kwa Simba na Yanga

Ni juu ya usajili wa wachezaji kabla dirisha halijafungwa

TFF yatoa onyo kwa Simba na Yanga

Ni juu ya usajili wa wachezaji kabla dirisha halijafungwa

12 July 2018 Thursday 10:31
TFF yatoa onyo kwa Simba na Yanga

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, TFF, limezipa onyo klabu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la kwanza, Ligi Daraja la Pili na Ligi Kuu Bara kuhakikisha zinakamilisha zoezi lake la usajili mapema ili kutoleta usumbufu hapo baadaye.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo, amesema TFF hawatoweza kuongeza siku zingine kwa ajili ya kufanya usajili hivyo ni vema klabu zote zikajitahidi kukamilisha zoezi hilo mapema.

Ikumbukwe dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15 2018 na klabu zote zikapewa semina ya mfumo mpya wa kufanya usajili kwa njia ya mtandano unaojulikana kama TFF FIFA CONNECT ambao utafungwa Julai 26 2018 saa 6 na dakika 59 usiku.

Ndimbo ametoa msisitizo wa klabu zote kuhakikisha wanakamilisha usajili kabla ya tarehe hiyo kutokana na baadhi zimekuwa zikiomba kuongezwa siku mbele jambo ambalo kwa sasa halitokuwepo.

Tayari timu mbalimbali haswa zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zimeanza zoezi hilo kwa kasi zikiimarisha vikosi vyao tayari kuelekea msimu mpya wa ligi unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti 2018.

Keywords:
TFFSimbaYanga
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.