banner68
banner58

TFF yazirahisishia Simba na Yanga kimataifa

TFF yazirahisishia Simba na Yanga kimataifa

13 July 2018 Friday 09:15
TFF yazirahisishia Simba na Yanga kimataifa

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha kanuni za kuruhusu usajili wa idadi ya Wachezaji 10 wa kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao.

Wachezaji hao wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja, katika Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka ambapo timu zilikuwa zinaruhusiwa kutumia wachezaji saba pekee wa kigeni.

Hayo yamewekwa hadharani mchana wa jana na Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia alipoitisha kikao na Waandishi wa Habari kuzungumzia mambo mbalimbali yanayogusia soka kwa ujumla.

Ongezeko hilo la wachezaji wa kigeni linaweza kuwa na faida kwa klabu ya Yanga ambayo ipo kwenye mashindano ya kimataifa pamoja na Simba pia Mtibwa Sugar ambazo zitakuwa zinashiriki michuano ya CAF msimu ujao kuanzia Disemba.

Mbali na maamuzi ya kuongeza wachezaji wa kigeni kutoka saba mpaka 10, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemthibitisha Kidao Wilfred kuwa Katibu Mkuu wa TFF katika kikao hicho kilichofanyika Julai 12,2018 Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala.

Kidao amechukua rasmi nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa na wadhifa huo, Selestine Mwesigwa ambaye ana kesi mahakamani inayohusiana na masuala ya utakatishaji fedha pamoja na aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Keywords:
TFFSimbaYanga
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.