banner68
banner58

Timu ipi duniani ina mashabiki wengi Afrika?

Azania Post itaungana nawe katika mjadala huo kuona timu ipi na kwa kigezo gani kinafanya iwe na mashabiki wengi

Timu ipi duniani ina mashabiki wengi Afrika?

Azania Post itaungana nawe katika mjadala huo kuona timu ipi na kwa kigezo gani kinafanya iwe na mashabiki wengi

17 May 2018 Thursday 16:48
Timu ipi duniani ina mashabiki wengi Afrika?

Na Amini Nyaungo

Wakati dirisha la usajili barani la majira ya joto huko Ulaya linatarajiwa kufunguliwa Juni 1, mashabiki wengi wanasubiria ni timu ipi itasajili wachezaji wazuri ili kuleta msisimko zaidi katika mbio za kuwania mataji mbalimbali msimu ujao.

Mashabiki wengi wa timu kama Arsenal kwa mfano, wamekuwa wanahamu kujua nani hasa atakabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha washika bunduki hao, na ni aina ya wachezaji atakaowasajili ili kuifanya timu hiyo kuwa na ushindani zaidi kwenye Ligi Kuu ya EPL ya England.

Tukiacha suala la usajili, kuna maswali mengi ya timu ipi ina wafuasi wengi zaidi duniani hususani katika bara la Afrika.

Azania Post itaungana nawe katika mjadala huo kuona timu ipi na kwa kigezo gani kinafanya iwe na mashabiki wengi haswa kwa Afrika.

Manchester United

Hii ni miongoni mwa klabu kubwa zaidi za soka ulimwenguni na imekuwa na ufuasi mkubwa, si barani Afrika pekee bali ulimwenguni kote.

Ukubwa wa kipato wa klabu hii ya kutoka jiji la Manchester nchini Uingereza kinaiwezesha kusajili wachezaji wazuri na wenye majina, japokuwa imeshindwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni, hasa baada ya kustaafu kwa kocha wake Sir Alex Ferguson.

Hakuna ubishi kwa Bara la Afrika, Manchester United inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi zaidi hii inatokana na historia ya timu hiyo kuchukua ubingwa pamoja na aina ya makocha waliopita hapo haswa kipindi cha Sir Alex Ferguson ndio kimepata wafuasi wengi sana.

Mara ya mwisho kuchukua kombe la ligi kuu Uingereza ilikuwa msimu wa 2012, bado inafanya vizuri sababu kizazi hiki kinazidi kuikuta inacheza vizuri inachukua makombe ikiwa ya FA na Europa.

Lazaro Masika huyu shabiki wa Mashetani wekundi mara zote anaitetea sana timu yake na atakubaliana na Azania Post juu ya wingi wa mashabiki.

Arsenal

Licha ya kutofanya vizuri kwa miaka 15 bado Arsenal imekaa katika nafasi ya pili kuwa na mashabiki wengi hapa Afrika na pia kwa ulimwenguni kote.

Wengi wamevutiwa na soka safi ambalo huonyeshwa na kikosi kilichokuwa chini ya Arsene Wenger, lakini ukitaka kuamini mfuate shabiki wa Manchester United muulize nani mpinzani wako wa jadi atakueleza kuwa Arsenal hii ilinogeshwa na Arsene Wenger na Alex Ferguson uwepo wao katika vikosi hivyo.

Demetrius Cleophace ni moja ya wapenzi wa Arsenal aliwahi kusema kuwa adui wake mkubwa ni Manchester united, huku Juventus Christopher akiwa hasimu mkubwa wa Demetrius.

Chelsea

Hapa sasa ndipo watu wataanza kuleta utata ila ukweli ni kwamba Chelsea inashika nafasi ya tatu kwa Afrika haswa kwa vijana ambao wameanza kuonja ladha ya mafanikio mwaka 2005 hivyo kufanya idadi ya mashabiki wa timu hii kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana.

Inawezekana baada ya misimu miwili endapo Arsenal ikifanya vibaya Chelesea itakaa katika nafasi ya pili kwani mashabiki wake wameongezeka kwa kasi kubwa sana.

Michael Nchila moja ya mashabiki wa Chelsea ukimueleza juu ya mpangilio huu ataweza akakataa na kutaka Chelsea ikae namba mbili ila ukweli unabaki kama ulivyo.

Liverpool

Moja ya timu kubwa nchini Uingereza, japo haiwezi kufikia timu kama Manchester United, Real Madrid na Barcelona, lakini kufifia kutofanya vizuri tangu 1990 kumefanya vijana wengi ambao waliozaliwa miaka ya 1990 hadi 2005 kutotaka kusikia na kujua kuwa Liverpool ni timu kubwa na yenye historia nzuri ya mafanikio.

Kwa sasa imezidiwa sana na timu nyingine za ligi kuu England tatizo kutofanya vizuri ligi kuu England hata michuano ya Ulaya japo ara mwisho walichukua 2005 kwa mshangao mkubwa.

Je wewe unaipangaje hii, ipi timu yako na unaona inastahili kukaa sehemu ipi.

Maoni ya muandishi

Hapo hazijawekwa Barcelona wala Real Madrid mashabiki wake kwa bara la Afrika ni wachache mno huwezi linganisha na timu hizo ambazo zimetajwa hapo juu, hivyo kwa bara hili Manchester United, Arsenal, Chelsea na Liverpool haswa zinakuwa na watu wengi sana.

Azania Post

Updated: 17.05.2018 18:46
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.