banner68
banner58

Ttesi za Usajili: Wachezaji wawili Gor Mahia sasa kumalizana na Simba dirisha dogo

Ttesi za Usajili: Wachezaji wawili Gor Mahia sasa kumalizana na Simba dirisha dogo

06 November 2018 Tuesday 00:00
Ttesi za Usajili: Wachezaji wawili Gor Mahia sasa kumalizana na Simba dirisha dogo

Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umeanza mchakato wa kuwania saini za wachezaji wawili kutoka Gor Mahia FC kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems anazihitaji.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza wachezaji Philemon Otieno na Ephrem Guikan ndiyo wanaowaniwa kwa ajili ya usajili pindi dirisha dogo litakapofungulowa Novemba 15 2018.

Wachezaji hao wawili wanacheza nafasi tofauti ambapo Guikan anakipiga katika nafasi ya ushambuliaji huku Otien akicheza nafasi ya kiungo.

Usajili huo umekuwa pendekezo la Aussems ambaye amedhamiria kukijenga kikosi cha Simba vema akiwa na malengo ya kukifikisha mbali pia kwenye mashindano ya kimataifa.

Mbali na wachezaji hao, ilielezwa pia Simba wataendelea kufukuzia saini ya Francis Kahata ambaye walianza kumnyemelea tangu msimu uliopita huku ikielezwa ana majina mengine pia ambayo atahitaji yasajiliwe.

Updated: 14.11.2018 15:27
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
samwel muha 2018-11-07 23:44:00

waje wapge kaz

Avatar
Nini 2018-11-06 14:08:07

Mpango huo ni mzuri sana hongera sana viongoxi

Avatar
Salumu Rashid 2018-11-08 18:56:09

Kwa Hapo Itakupoa

Avatar
johnbosco haule 2018-11-12 16:49:25

kocha ausems anamalengo na simba viongoz wa simba wampe ushirikiano