banner68
banner58

Tuzo za Mo: Jonas Mkude na Shiza Kichuya wawagawa mashabiki wa Simba

Watofautiana juu ya nani alistahili kupata tuzo

Tuzo za Mo: Jonas Mkude na Shiza Kichuya wawagawa mashabiki wa Simba

Watofautiana juu ya nani alistahili kupata tuzo

13 June 2018 Wednesday 13:11
Tuzo za Mo: Jonas Mkude na Shiza Kichuya wawagawa mashabiki wa Simba

Na Amini Nyaungo

Kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwa mashabiki wa Simba baada ya tuzo za muwekezaji Mkuu wa timu hiyo, Mohamed Dewji amezitoa kwa wachezaji na watu mbalimbali wanaohusika na timu hiyo kutokana na mchango wao kuelekea mafanikio ya timu hiyo.

Mgawanyiko uliopo juu ya tuzo ya Kichuya wakati huo kipenzi chao Jonas Mkude akikosa, wengi wanalalamika kuwa hajatendewa haki na kwamba alistahili kuipata yeye na wala si Kichuya.

Kundi la wengine wengi wakitoa uhalisia wa tuzo hizo akiwemo Ayoub Mbowe kuwa kutokana na Kichuya kuwa amecheza mechi nyingi na hivyo kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chake kwa msimu mzima na kwa makocha wote ambao wamekuwa na timu hiyo kwa kipindi hicho, Joseph Omog na Pierre Lichantree, huku Jonas Mkude akiwa amecheza zaidi kipindi cha Lichantree licha ya kufanya kazi nzuri.

"Ni sahihi kabisa Kichuya kupata tuzo hiyo, wote bora ila winga huyo amecheza mechi nyingi na amesaidia sana timu,'' amesema shabiki huyo wa Wekundu wa Msimbazi.

Aliyeibua mjadala huo ni Johnson Benard akiwalaumu wenzake kushikilia mzozo huo kana kwamba hakuna kitu kingine cha kuelezea, yeye pia amesema Mkude alistahili kukosa tuzo hiyo.

Akisema kuwa "Kukosa tuzo kwa Jonas Mkude ni sahihi tu kwa sababu wewe unaelalamika je ulimpigia kura? Sio kwamba hana uwezo ila ulimpigia kura?” alihoji.

"Kwangu mimi naona ni sawa tu kwa sababu sikumpigia kura mtu yeyote kwa hiyo siwezi kulalamika maana kutokupiga kura kwangu ndiko kulikomfanya mtu fulani apungukiwe na wingi wa kura, labda kura yangu ingempa ushindi Shomari Kapombe au Emmanuel Mseja," aliongeza.

 Mwisho amewamambia kuwa watafute habari nyingine hiyo ya Mkude imewachosha na inalenga kuharibu umoja walionao, wanatakiwa kuheshimu kilichoamuliwa.

Nawewe unaweza kuchangia juu ya mjadala huu ambao umekuwa mkubwa sana, unahisi Nani anastahili kuwa kiungo Bora wa mwaka wa Simba Kati ya Kichuya na Mkude, tunatumia Azania Post Facebook, Instagram na Twitter.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
KASTOL MWENDA KUTOKA SONGEA MADABA 2018-08-02 09:38:59

Kwam tazamo wangu naona mkude alistahli kupata tuzo hyo walasi kichuya