UEFA LIGI: Liverpool, Chelsea, Barcelona zatakata

UEFA LIGI: Liverpool, Chelsea, Barcelona zatakata

03 October 2019 Thursday 06:00
UEFA LIGI: Liverpool, Chelsea, Barcelona zatakata

MECHI za makundi ya ligi ya UEFA Championi ligi zimeendelea tena usiku wa kuamkia Oktoba 3, 2019 na kushuhudia Liverpool, Barcelona na Chelsea zikipata ushindi.

Wakiwa nyumbani katika uwanja wa Nou Camp, Barcelona walilazimika kupambana vya kutosha ili kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Inter Milan ya Antonie Conte.

Kwani kunako dakika ya pili ya kipindi cha kwanza Inter Milan kupitia kwa mchezaji Lautaro Martinez iliandika bao la kuongoza lakini kunako kipindi cha pili dakika ya 58 mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez aliisawazishia timu yake hiyo. Pia kunako dakika 85 Muuruguy huyo aliindika timu yake bao la pili na la ushindi.

Mchezo wa kwanza Barcelona walitoka sare ya 0-0 dhidi ya Borussia Dortmund

Barcelona sasa wapo nafasi ya pili kwa kuwa na pointi nne katika kundi lao sawa na Dortmund inayoongoza wakati Inter Milan na Slavia Praha wakiwa na point moja moja kila mmoja

Updated: 03.10.2019 06:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.