UEFA Ligi:Spurs yafungwa 7-2, Juve yatakata

UEFA Ligi:Spurs yafungwa 7-2, Juve yatakata

02 October 2019 Wednesday 06:10
UEFA Ligi:Spurs yafungwa 7-2, Juve yatakata

MECHI za makundi ya michuano ya UEFA championi ligi imechezwa usiku wa kuamkia Oktoba 2, 2019.

Katika mechi nane zilizochezwa timu ya Tottenham Hotspurs ikiwa nyumbani nchini Uingereza imefungwa goli 7-2 na Buyern Munich ya Ujerumani.

Tottenham ambaye msimu wa 2018/19 ilishika nafasi ya pili ya mashindani ya UEFA championi ligi nyuma ya Liverpool ilianza kupokea mvua hiyo ya magoli kunako dakika 15 kupitia beki wa Buyern, Joshua Kimmich.

Mshambuliaji ambaye sasa yupo katika kiwango Robert Lewandowski alifunga magoli mawili dakika ya 45 na 87 pamoja na Serge Gnabry aliyefunga magoli manne dakika ya 53, 55, 83 na 88 na kuufanya mchezo umalizike kwa magoli 7-2, huku Spurs wakifunga mawili kupitia kwa Son Heung-Min dakika ya 12 na Harry Kane kwa mkwaju wa penati dakika ya 61.

Kipigo hicho cha kihistoria kinaifanya Tottenham Hospurs kuingia katika rekodi mbaya kwa kuwa ndio kipigo chao kikubwa cha kwanza katika historia yao kufungwa wakiwa nyumbani.

Haya hapa matokeo kamili :

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.