UEFA waongeza michuano ya vilabu Ulaya

UEFA waongeza michuano ya vilabu Ulaya

25 September 2019 Wednesday 07:17
UEFA waongeza michuano ya vilabu Ulaya

SHIRIKISHO la soka barani Ulaya (UEFA) usiku wa kuamkia leo Septemba 25, 2019 limetangaza viwanja vitakavyotumika kuwa mwenyeji wa michezo ya fainali ya UEFA Champions League kwa misimu kadhaa ikiwemo msimu wa 2020/2021.

Pia, UEFA imetaja jina la michuano ya tatu ya vilabu Ulaya itakayoanzishwa na kuanza kuchezwa mwaka 2021, itaitwa UEFA Conference.

UEFA imetangaza viwanja vitatu mwenyeji wa fainali zijazo za UEFA Champions League.

UEFA imetangaza kuwa msimu wa 2019/2020 mchezo wa fainali ya UEFA Champions League utachezwa Atatürk Olimpiyat Stadı nchini Uturuki katika mji wa Istanbul, wakati msimu unaofuatia wa 2020/2021 mchezo huo utachezwa katika uwanja wa St Petersburg.

Huku faina ya waka 2021/2022 itachezwa Allianz Arena nchini Ujerumani na 2022/2023 utachezwa Wembley London England.

Uamuzi huo umetangazwa katika mkutano wa kamati ya UEFA uliyofanyika Slovenia na kwamba maamuzi hayo yameangalia vitu vingi ikiwemo hoteli, miundombinu na ufikaji wa mashabiki kirahisi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.