Unayotakiwa kujua kuhusu Afcon

Unayotakiwa kujua kuhusu Afcon

14 June 2019 Friday 14:51
Unayotakiwa kujua kuhusu Afcon

MASHINDANO ya Afcon 2019 yanatarajia kuanza rasmi Juni 21,2019  nchini Misri. Timu zishiriki katika mashindano hayo ikiwemo Taifa Star ya Tanzania zimeshawasili nchini humo.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayopaswa kujua kuhusu Afcon; 

 - Misri itaandaa kwa mara ya tano kombe la Afcon. Walikuwa wenyeji wa kombe hilo 1959, 1974, 1986 na 2006, wakaibuka washindi katika michuano minne na kumaliza katika nafasi ya tatu katika mchuano wa mwisho.

 - Ni mataifa matatu pekee, wenyeji Misri, Sudan na Ethiopia walioshiriki katika mchuano wa kwanza mnamo mwezi Februari 1957 na kulikuwa hakuna michuano ya kufuzu.

 - 2019 Itakuwa michuano ya  kwa kwanza itakayoshirikisha mechi 24 , baada ya Caf kuamua kupanua mchuano hiyo ili kuimarisha ushindani.

 - Taifa lililofanikiwa zaidi katika mashindano hayo ni Misri ikiwa na mataji saba ,ikifuatiwa na Cameroon {5} Ghana {4} Nigeria {3} , DR Congo na Ivory Coast {2 kila mmoja wao}

 - Madagascar, Burundi na Mauritania zitakuwa zikishiriki kwa mara ya kwanza . Timu 12 hazajiwahi kufuzu katika kinyang'anyiro hicho , ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, Chad Comoro, Djibouti, Eritrea, Eswatini, Gambia, Lesotho, São Tomé and Príncipe, Seychelles, Somalia na Sudan Kusini.

 - Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto'o anaongoza kwa wingi wa magoli, baada ya kufunga magoli 18 katika michuano 18 kati ya  mwaka 2000 na 2010.

 - Kipa wa Misri Essam el Hadary ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa akiwa na miaka 44 na siku 21 kushiriki katika michuao hiyo wakati alipocheza dhidi ya Cameroon mwaka 2017 mjini Libreville.

 - Shiva N'zigou wa Gabon ndio mchezaji wa umri mdogo zaidi kushiriki na kufunga katika michuano hiyo. Alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 93 wakati aliposhiriki katika michuano ya Afcon ya 2000 akifunga katika kichapo cha 1-3 dhidi ya Afrika Kusini

 - Mchuano huo umebadilishwa siku zake za kufanyika ili kuzuia kugongana na kombe la dunia. Afcon kwa mara ya kwanza mwaka huu itafanyika katikati ya mwaka kinyume na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa ikifanyika mwezi Januari ili kuzuia mgongano wa mataifa na klabu za Yuropa.

- Mataji matatu tofauti yamekabidhiwa washindi katika historia ya michuno hiyo. Kombe la sasa lilikabidhiwa  mwaka 2002 na Misri iliibuka mshindi wakati huo baada ya kukamilisha ushindi wao wa mataji matatu  mwaka 2010.

BBC

Updated: 15.06.2019 08:11
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.