Uongozi Simba watoa tamko jingine juu ya kocha Masoud Djuma

Uongozi Simba watoa tamko jingine juu ya kocha Masoud Djuma

17 September 2018 Monday 08:02
Uongozi Simba watoa tamko jingine juu ya kocha Masoud Djuma

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kukosekana kwa Kocha wake Msaidizi, Mrundi Masoud Djuma, si sababu ya timu hiyo kwenda suluhu na Ndanda FC.

Simba ilikuwa na kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumamosi ya wiki jana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona ambao ulimalizika kwa suluhu tasa ya 0-0.

Manara amesema kukosekana kwa Djuma hakujabadilisha chochote na hata kama angekuwa matokeo ya aina yoyote ile yangeweza kupatikana.

"Kukosekana kwa Djuma si sababu ya sisi kwenda suluhu na Ndanda, katika mchezo wa mpira kunakuwa na aina ya matokeo matatu, sidhani kama wanaotupia lawama suala la yeye kubakia Dar es Salaam wanafanya jambo jema" alisema.

Ofisa huyo ameeleza kuwa Djuma alisalia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya kazi kwa kuwanoa wachezaji ambao hawakuambatana na kikosi kuelekea Mtwara kwa ajili ya mechi hiyo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.