banner68
banner58

Uongozi Yanga waweka tofauti juu ya kikosi cha sasa na msimu uliopita

Uongozi Yanga waweka tofauti juu ya kikosi cha sasa na msimu uliopita

16 September 2018 Sunday 07:51
Uongozi Yanga waweka tofauti juu ya kikosi cha sasa na msimu uliopita

Wakati kikosi cha Yanga kikiwa tayari kushuka dimbani taifa leo kukipiga na Stand United, uongozi wa klabu hiyo umesema aina ya wachezaji walionao kwa sasa hawana utofauti zaidi na wa msimu uliopita.

kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili pamoja Kamati ya Mashindano, Hussein Nyika, amesema kikosi chao kina mchanganyiko wa wachezaji wenye uazoefu na vijana.

Nyika ameeleza kuwa Yanga ya sasa na msimu uliopita haina utofauti mkubwa kiasi cha kwamba inaweza ikatofautishwa bali wachezaji waliopo ni wale wakongwe pamoja na vijana.

"Kikosi ni kilekile, hakuna utofauti zaidi na msimu uliopita kwa maana tuna wachezaji vijana na wakongwe ambao wamekuwa wakishirikiana kwa namna moja ama nyingine kuisaidia timu kupata matokeo uwanjani," alisema.

Yanga inashuka Uwanja wa taifa majira ya saa 12 jioni kukipiga na Stand United ambao tayari wana siku kadhaa hapa Dar es Salaam kusubiria mechi hiyo.

Updated: 16.09.2018 07:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.