Usajili uliokamilika : Kutana na usajili bora kabisa Simba

Usajili uliokamilika : Kutana na usajili bora kabisa Simba

16 June 2018 Saturday 16:30
Usajili uliokamilika : Kutana na usajili bora kabisa Simba

Na Amini Nyaungo

Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Juni 1, timu mbalimbali zimefanya usajili wake zikiwa na malengo ya kuziba nafasi zilionekana hazijafanya vizuri msimu uliopita.

Azania post inakupa usajili wa Simba ambao tayari umekamilika na wengine washaanza kucheza huku tetesi zikiendelea katika klabu hiyo.

Kwa aina ya wachezaji waliosajiliwa wengi wanasema kuwa ni wafungaji bora wa timu zao walipotoka, na hizi ndio takwimu zao katika vilabu husika.

Adam Salamba

Mchezaji wa zamani wa Lipuli amejiunga na Simba msimu huu kwa ada ya uhamisho inayosemwa ni milioni 40 pamoja na usafiri wa gari.

Salamba alifunga magoli 6 akitoa nafasi za goli 3 katika timu yake ya zamani, kocha akiwa Amri Said na Suleiman Matola.

Alicheza michuano ya Sports Pesa Super Cup jumla ya   dakika 51. Hakufunga goli ila bado mchezaji mahiri na msaada mkubwa kwa Simba.

Marcel Kaheza

Ametokea Majimaji ya Songea moja ya washambuliaji hatari sana, walisumbua, mfungaji bora namba 3 akifunga magoli 14 akiwa sawa na John Bocco.

Mchezaji mahiri endapo Simba watamtumia vizuri, kituko pale alipocheza dakika  20 katika kipindi cha pili kisha kutolewa.

Mohamed Rashid

Alicheza Tanzania Prisons alifanya vizuri sana huku akifunga magoli 9, moja ya washambuliaji wazawa waliofanya vizuri sana, yeye bado  amecheza ila hajaonesha makali yake ni muda na kuzoea mazingira ya klabu kubwa kama Simba.

Updated: 17.06.2018 12:16
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Usajili Wa Simba 2019 2019-06-12 21:04:46

Simba